Na Bertha Ismail-
Arusha
Jeshi la
polisi mkoani Arusha, limemfikisha
mahakamani mtuhumiwa wa ugaidi, Victor Ambros Kalist (20) mwendesha boda boda
mkazi wa Kwa Morombo jijini hapa na kuwaachia huru Raia wanne kutoka nchi za
falme za kiarabu ambao waliingia nchini Mei 4 mwaka huu,baada ya kubaini kuwa
hawausiki na tukio hilo.
Akisoma
mashitaka mbele ya hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya wilaya , Arusha, Devota
Kamuzola, mwendesha mashitaka wa serikali Zacharia,akiwasaidiwa na Haruna Matagane
na SC Ndomba,alisema kuwa mshitakiwa, Ambros
anashitakiwa kwa makosa 21 yakiwemo matatu ya kuuwa na 18 ya kujaribu kuuwa .
Alisema kuwa
mnamo Mei 5 mwaka huu huko maeneo ya Olasiti majira ya saa4.30 katika kanisa la
Mt. Joseph mfanyakazi, Ambros aliua watu
watatu, Partisia Joakim,Regina Lining’o na James Kessy kinyume cha kifungu namba
196 cha sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 kama ilivyofanyiwa maboresho
mwaka 2002.
Akisoma
shtaka la pili alisema Ambros alijaribu kuuwa watu 18 kinyume cha kifungu namba
211(a) cha sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 kama ilivyofanyiwa maboresho
mwaka 2002.
Aidha katika
shauri hilo la jinai namba 18 ya mwaka 2013, mshitakiwa hakutakiwa kujibu
chochote na kurudishwa rumande hadi kesi yake itakapotajwa tena mahakamani
hapo.
Akizungumzia
kufikishwa mahakamani kwa mtuhumiwa huyo kamanda wa polisi mkoa wa Arusha
Liberatus Sabas alisema kuwa jeshi la polisi kwa kushirikiana na ofisi ya
mwanasheria mkuu wa serikali limejiridhisha na ushahidi walioupata na
kumfikisha mahakani.
Hata hivyo
kamanda Sabasi aliwataja raia wanne wa kigeni toka nchi za falme za
Kiarabu (UAE) walioachiwa huru na
kurudishwa makwao kuwa ni Abdul Azizi
Mubarak (30)ambae ni mfanyakazi wa mamlaka ya mapato katika falme hizo na
mwingine ni Fouad Saleem Ahmed Al Hareez AL Mahri (29) ambae ni mfanyakazi kikosi
cha zima moto.
Wengine ni
Saeed Abdulla Saad (28) ambae ni skari polisi kitengo cha trefik karika falme
hizo pamoja na Raia mmoja wa Saudi Arabia Al-Mahri Saeed Mohseens (29).
Aidha
aliendelea kueleza kuwa uchunguzi wa kina unaofanywa na timu ya upelelezi
ukihusisha taasisi zingine za upelelezi FBI pamoja na Interpol kuhusiana na mlipuko wa bomu bado
unaendelea kuwahoji watuhumiwa wengine kati ya 9 waliokuwa wanashikiliwa.
0 comments:
Post a Comment