Na Juma Mtanda, Morogoro
MKUU
wa wilaya ya Mvomero, Anthony Mtaka amezindua mradi wa maji na usafi wa
mazingira kwa shule za msingi Mlali na Vitonga wenye thamani ya
Sh72.7milioni ukiwemo wa uvunaji wa maji ya mvua katika kata ya Mlali
mkoani Morogoro.
Mradi
huo umetekelezwa na shirika la Environmetal Conservation, Water
Sanitation and Aids Control Organization (EWACO) kwa ufadhili wa shirika
la WaterCan na wananchi wa vijiji vya Mlali na Vitonga.
Akizungumza
na wananchi katika mkutano wa hadhara kwa nyakati tofauti katika vijiji
vya Mlali na Vitonga, Mtaka alisema kuwa shirika la EWACO limeondoa
moja ya kero ya muda mrefu ya shule za msingi Mlali na Vitonga kwa
kujenga miradi hiyo yenye thamani ya Sh 72.7 milioni.
Alisema
kuwa ili miradi hiyo iweze kuendelea kudumu ni lazima walimu, wanafunzi
na wakazi wa eneo hilo kutunza miundombinu yake ili iendelee kuleta
faida kwa walengwa.
Shirika
Ewaco linapwa kuigwa na mashirika mengine kutokana na utendaji wao
kwani thamani ya fedha iliyotajwa inafafana na thamani ya miradi
iliyotekelezwa. Alisema Mtaka.
Naye
Mratibu wa Shirika hilo, Stanley Shekigenda alisema kuwa shirika hilo
imetekeleza miradi miwili ya uvunaji wa maji ya mvua na ujenzi wa vyoo katika shule za msingi Vitonga na Mlali kwa ufadhili wa shirika la WaterCan pamoja na kushirikiana na wananchi.
Shekigenda
alitolea ufafanuzi wa fedha zilizotumika kwenye miradi hiyo kuwa ni
pamoja na ujenzi wa shule ya msingi ya Mlali uliogharimu Sh46,6 milioni
na shule ya Vitonga kiasi cha Sh26.1 milioni mbali na fedha kutoka EWACO
pia wananchi wa Mlali imechangia kiasi cha Sh4.9 milioni na wale wa
kijiji cha Vitonga wamechangia Sh2 milioni.
Shekigenda
alisema kuwa ujenzi wa mantaki mawili ya uvunaji wa maji ya mvua yenye
ujazo wa lita 110,000 yaliyojengwa katika shule ya msingi ya Mlali na
matundu 20 ya vyoo vya walimu na wanafunzi, wakati shule ya msingi
Vitonga likijengwa tanki la lita 56,000 na ujenzi wa matundu 17 ya vyoo
kwa walimu na wanafunzi.
Mwisho…
0 comments:
Post a Comment