.

.
Saturday, May 25, 2013Nyumba pamoja na gari la mtangazaji wa kituo cha Televisheni cha Taifa TBC imechomwa moto juzi katika vurugu za Mtwara

Akizungumza katika mahojiano hayo mtangazaji huyo aliweka wazi sababu za nyumba yake kuchomwa moto kuwa ni kutokana na kazi anayoifanya mke wake.


Alisema kuwa mke wake ni polisi hivyo inawezekana ndiyo sababu kubwa iliyochangia kuvamiwa na kuchomewa nyumba yake moto pamoja na gari

Alisema kazi yake pia ni sababu ya pili iliyochangia kuvamiwa kwani vurugu za mara ya kwanza alikatazwa kuandikwa chochote juu ya vurugu hizo

Wakati huo huo jeshi la polisi limewashikiria watu 91 wanaodhaniwa kushawishi vurugu zilizotokea juzi mkoani Mtwara.

Akizungumza katika mahojiano maalumu katika kipindi kimoja wapo cha radio jijini Dar es Salaam Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Mtwara alisema hali ya usalama inazidi kuimalisha ingawa bado wananchi wa mkoa huo hawajajitokeza kuendelea kufanya kazi zao za kijamii.

Alisema kuwa maeneo ya Magomeni ndiyo yaliyoharibiwa na vurugu hizo ingawa vurugu hizo zilianzia sokoni

0 comments:

Post a Comment