.

.
Tuesday, May 21, 2013

7:38 AM
WIKI iliyopita niliulizwa swali kama majini wanazaa? Jibu ni kwamba  wanaoana na kuongezeka kama tulivyo binadamu na huzaana kwa wingi sana.
Binadamu mwanamume ana uwezo wa kumuoa jini mwanamke na jini wa kiume ana uwezo wa kumuoa binadamu mwanamke pamoja na kwamba ndoa inayotambulika na Mwenyezi Mungu ni ya kiumbe kwa kiumbe yaani binadamu kwa binadamu na jini kwa jini.
Majini na mashetani nao wanakufa isipokuwa wao wanaishi miaka mingi kuliko binadamu kwa sababu hawana maumbo maalum.
MARAFIKI WA MAJINI
Majini huwa wanafanya urafiki na binadamu lakini marafiki wao wakubwa ni ngamia. Baadhi yao wanaishi katika nyumba tunazoishi na ukitaka kuwafukuza unasoma Quran au Biblia au kumtaja Mwenyezi Mungu.
Majini hukusanyika na kuongezeka giza linapoingia au unapopatwa mwezi, na huwa wanakimbia wanaposikia Adhana au Kengele ya kamba.
Majini wengi wanapenda kukaa penye kivuli cha miti mikubwa kama mibuyu na ujue kuwa siyo vizuri kukaa eneo hilo.
SURA ZA MAJINI NA MASHETANI:
Majini sura zao ni za kutisha na mfano wake ni kama matunda ya mti wa Zaqum ambao unatoa matunda yenye sura mbaya na yanayofanana na mawe.
Majini wanakuwa na mkutano kila siku nyakati za kuchomoza na kuzama jua na nyakati hizo ndizo ambazo wanafanya maasi yao.
Fitina na maasi yao mengi wanafanyia upande wa Mashariki. Majini vilevile wanaweza kujigeuza kama mbwa mweusi au paka mweusi kwa sababu wanapenda gi nyeusi kwa sababu ya kiza.

0 comments:

Post a Comment