Lwakatare akimkumbatia kwa furaha wakili wake, Peter Kibatara, baada ya kufutiwa mashitaka ya ugaidi.
Askari wakimuamuru Lwakatare kuondoka kizimbani kwa ajili ya safari ya gerezani.
Ndugu, jamaa na wafuasi wa Chadema wakikumbatiana kwa furaha.
Mmoja wa wanachama wa Chadema akiwapigia simu wenzake kuwapasha kilichojiri mahakamani.
Ulinzi nje ya jengo la mahakama.
Wafuasi wa Chadema wakitoka mahakamani kwa furaha.
Kibatara akifafanua jambo kutoka kwenye makabrasha yake
Lwakatare akirudishwa rumande kwa kosa moja la kutaka kumwekea sumu, Dennis Msaki.
Taarifa kutoka Mahakama Kuu zinasema Mahakama Kuu imebakiza shitaka moja tu, la utekaji ambalo kimsingi ni Jinai na lina dhamana.
Taarifa zaidi zinasema ni shangwe kuu kutoka kwa wafuasi wa CHADEMA walioko mahakamani na Familia ya Lwakatare.Baadhi ya wafuasi wa CHADEMA waliohoj
iwa wamesema huu ni ushindi mkubwa dhidi ya udhalimu.
Mwanafamilia mmoja wa Lwakatare huku akibubujikwa machozi akasema mkono wa Mungu umeonekana dhidi ya shetani mtoa roho za watu.
Katika kesi hii Lwakatare anawakilishwa na Jopo la mawakili nguli watano ambao ni Mabere Marando,Tundu Lissu,Professor Abdallah Safari,Peter Kibatala na Naronyo Kicheere.
0 comments:
Post a Comment