WANANCHI Mkoani Mtwara wameamua kuingia barabarani na kuanza
kufanya fujo zilizopelekea polisi kuanza kufyatua mabomu ya machozi kwa ajili
ya kuwatawanya waandamanaji hao wanaoshindana na serikali kwa miezi kadhaa
sasa.
Awali, wananchi wote mkoani Mtwara siku ya leo ilikuwa kufuatilia
mambo ya Bunge yanavyokwenda, huku wakiwa na hamu ya kuona nini kitaamuliwa
katika Bajeti ya Muhongo, wakitaka kuona mkoa wao unapendelewa zaidi kwa uwapo
wa gesi.
Baada ya kuona bajeti hiyo ipo tofauti na dhamira yao, waliamua
kurudi tena kwenye harakati zao kwa ajili ya kushinikiza malengo yao kwa
serikali juu ya gesi.
Hadi sasa, mabomu yanaendelea kulipuliwa mjini hapa na wengi
wasiokuwa na uwezo wa kushi
riki, hasa wazee wakiwa wamejichimbia majumbani
mwao.
Sera ya mkoani Mtwara ni gesi kwanza, uhai baadaye, moja ya kauli
mbiu zinazotumika kuwapa kiburi wananchi. Tangu kuzuiwa kufanyika kwa mikutano
ya hadhara, wananchi wanatumia mbinu mpya ya kuhamasishana kwa njia ya meseji
na vipeperushi na wakati mwingine kwa njia ya usafiri wa umma na kwenye maduka.
0 comments:
Post a Comment