Na Bertha ismail-Ngorongoro
MIILI mitatu ya
watanzania wa jamii ya Kisonjo waliouwawa katika eneo la Narok wilayani Kajiado
nchini Kenya imeingia katika sura mpya mara baada ya Serikali ya Tanzania
kushindwa kuirejesha nchini miili hiyo huku serikali ya Kenya ikidai kuwa
hawakuwa watanzania
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi mkoa
wa Arusha Liberatus Sabas alisema kuwa tayari mtu mmoja ambaye ni askari polisi
anashikiliwa na jeshi hilo kwa uchunguzi zaidi ingawaje alisema kwa sasa jina
la askari huyo linahifadhiwa kwa ajili ya upelelezi
Sabas alisema kuwa wanamshikilia askari huyo kwa kosa la
upotevu wa silaha ambayo inasadikiwa kuwa ilitumika katika tukio uhalifu
linalohusishwa na mauji ya vijana hao watatu wa Kitanzania nchini Kenya.
Kuhusu Marehemu hao, kamanda amesema kuwa Serikali ya Kenya
kupitia Jeshi lake la polisi ndio wanajukumu la kurejesha Miili yao hapa nchini .
Awali Msemaji wa familia tatu za marehemu hao,Pasto Webo
alidai kuwa askari wa kituo cha polisi Loliondo waliwatoza kiasi Milioni mbili
na nusu kwa ikiwa kama gharama za kuwasafirisha marehemu kutoka kenya kwa gari
la Polisi kwa kiwango cha shilingi laki nane kwa kila mwili mmoja.
Lakini Kamanda wa Polisi alisema kuwa Jeshi hilo halina
utaratibu wa kusafirisha marehemu na kwamba anafuatilia madai hayo na
itakapobainika kuwa ni kweli watachukuliwa hatua kali za kisheria.
Kuhusu kuhusika kwa polisi wa loliondo na kupotea kwa vijana
wao watatu msemaji wa familia hizo tatu alidai kuwa May tatu mtoto wake ambaye
ni Tibiti webo alikuja nyumbani kwake akiwa na askari polisi ambaye anajulikana
kwa jina la Lazaro ambapo walikula chakula na walipoondoka kwa pamoja kijana
huyo hakuonekana tena.
Pia alidai inasemekana kuwa kijana huyo alimpitia rafiki yake ambaye amejulikana kwa jina la
Kadogo anna ambapo tangu alipoondoka
tarehe tatu mwezi huu hawakuonekana tena
mpaka hivi karibuni polisi
walipowaletea ripoti pamoja na picha kuwa vijana wao wameuwawa vibaya Narok
“tulipotazama hizo picha tuliweza kuwatambua vijana wetu
wawili lakini pia alikuwepo mwingine wa
tatu ambaye tunadhani kuwa anatokea kijiji cha jirani”
Inadaiwa kuwa polisi waliwaeleza kuwa vijana wao waliuwawa
katika tukio la ujambazi katika eneo la
Narrok ambapo ilidaiwa kuwa waliwavamia
wafanyabiashara kwa ajili ya kuwapora fedha lakini wakauwawa na wananchi wenye
hasira kali
Katika tukio hilo vijana hao walikutwa na silaha ambayo
inaaminika kuwa walipewa na askari wa kituo cha polisi cha loliondo.
Akizungumza kwa njia ya simu kutoka Dar es salam balozi wa
Kenya Nchini Tanzania ,Mutinda Mutiso alidai kuwa vijana waliouwa sio
watanzania bali ni wa Kenya huku akiongeza kuwa tukio hilo lilitokea wakati
yeye akiwa nchini humo.
Hataivyo wazazi wa marehemu hao wanasisitiza kuwa vijana hao
ni watanzania na ni lazima miili yao iweze kurejeshwa miili hiyo kwa taratibu za maziko hapa nchini
ingawaje Serikali ya Kenya ilitaka kuzika miili hiyo nchini humo kama
wangefanikiwa kupata saini ya ndugu wa
marehemu
|
0 comments:
Post a Comment