Mbunge
wa jimbo la Iringa mjini -Chadema mchungaji Peter Msigwa akiwa amebebwa
na mashabiki wa chadema nje ya mahakama muda mfupi baada ya kuachiwa
kwa dhamana jana.Picha na Habari na Chadema
SAKATA
la vurugu za machinga na polisi mjini Iringa limechukua sura mpya baada
ya jeshi la polisi mkoa wa Iringa kumfikisha mahakamani mbunge wa jimbo
la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa pamoja na watuhumiwa wengine
zaidi ya 70
Huku
mahakama hiyo ikitoa masharti nafuu ya dhamana kwa watuhumiwa hao na
kuwaonya kutofanya kosa kwa kipindi chote cha kesi hiyo inapoendelea
kusikilizwa .
Watuhumiwa
hao walifikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi wa wilaya ya Iringa
Mheshimiwa Godfrey Isaya jana majira ya saa 8 mchana huku wakiwa chini
ya ulinzi mkali wa askari wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) waliokuwa
na msafara wa magari zaidi ya matatu likiwemo gari ya maji ya kuwasha .
Mbali ya
mbunge Msigwa kupanda gari ndogo ya wazi ya polisi pamoja na watuhumiwa
wawili wanawake waliokamatwa katika vurugu hizo bado watuhumiwa wengine
74 walitumia usafiri wa karandinga la polisi .
Mbele ya
mahakama hiyo wakili wa serikali Adolph Maganda alisema kuwa watuhumiwa
hao kwa pamoja wanatuhumiwa kwa kosa kwa makosa matatu likiwemo la
kufanya kushiriki mkutano na kufanya vurugu ,uchechezi na kuharibu mali
kinyume na sheria
Huku mbunge akisomewa mashitaka mawili likiwemo kushawishi na kufanya mkutano bila kibali .
Watuhumiwa
wote wamekana mashitaka dhidi yao huku wakili wa serikali akidai kuwa
hana pingamizi na dhamana kwa watuhumiwa hao wote hata hivyo wote
wamekana mashitaka yote yaliyotolewa dhidi yao .
Hata hivyo
makimu anayesikiliza kesi hiyo alisema kuwa dhamana kwa washitakiwa wote
ipo wazi kwa kila mmoja kuwa mdhamini mmoja anayeaminika pamoja na
kusaini hati ya dhamana ya Tsh milioni moja .
Hadi majira
ya saa 10 jioni mahakama hiyo ilikuwa ikiendelea na mchakato wa kupitia
barua za dhamana kwa wadhamini huku mbunge akiwa wa kwanza kudhaminiwa
,mbali ya mbunge watuhumiwa kati ya 74 waliokuwa bado kupata wadhamnini
ni watuhumiwa sita pekee.
Katibu wa
chama cha Demokrasia na maendeleo (Chadema) wilaya ya Iringa mjini
Suzana Mgonakulima alisema kuwa mchakato wa kuwadhamini watuhumiwa wote
waliosalia unaendelea kufanyika na kuwa wana uhakika wa watuhumiwa wote
kudhaminiwa .
Hadi majira
haya ya saa 10 .40 mbunge msigwa na wengine wameachiwa huku watuhumiwa
26 kati ya 74 wamekosa dhamana hadi kesi hiyo itakapotajwa tena tarehe 3
/6/2012
Wakati huo
huo wananachi waliofika mahakamani hapo kushuhudia mbunge wao
akifikishwa mahakamani wamempongeza mkuu wa kikosi cha kutuliza ghasia
mkoa wa Iringa (FFU) Said Abdulah Mnunka kwa kusimamia amani na utulivu
katika eneo hilo la mahakama na jinsi ambavyo alivyoweza kupambana na
machinga pasipo kumwaga damu kwa siku ya jana wakati wa vurugu hizo
chanzo: lineneke blog
0 comments:
Post a Comment