.

.
Wednesday, May 8, 2013

7:38 AM

http://www.mtanzania.co.tz

Mh. Waziri Wa Ulinzi na Jeshi La Kujenga Taifa Mh. Shamsi Vuai Nahodha.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi.

SASA ni wazi kuna kila dalili zinazoonyesha nchi ipo katikati ya tishio la ugaidi kutokana na matukio ambayo tayari yameshuhudiwa, likiwemo lile la ulipuaji bomu katika Kanisa la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi lililotokea mkoani Arusha hivi karibuni. 

Kuibuka kwa matukio makubwa ambayo hayakuwahi kushuhudiwa katika siku za nyuma ya kuuwawa kwa viongozi wa dini, kumwagiwa tindikali, kuchoma makanisa, kuteka na kujeruhi watu maarufu ni dalili za wazi kwamba nchi imegubikwa na tishio hilo la ugaidi.

Taarifa zilizolifikia gazeti hili zinaeleza kuwa, kuibuka kwa vitendo hivyo kunachangiwa na sababu nyingi, kubwa ikiwa ni ile ya nchi za Ulaya kutumia kivuli cha ugaidi na kile cha kulinda amani (Peace Keeping) kwa sababu ya maslahi yake binafsi na ya kiuc
humi.

Pamoja na hilo, sababu nyingine inayotajwa ni Mamlaka husika kushutumiwa kushindwa kudhibiti wageni wanaoingia na kutoka hali ambayo imekuwa ikitoa fursa ya wageni wengi kuingia na kuishi nchini kiholela pasipo sababu za uwepo wao nchini kufahamika.

MKAKATI WA MATAIFA MAKUBWA
Mkakati unaodaiwa kuratibiwa kwa nyuma na nchi zenye nguvu ya kiuchumi duniani kwa kivuli cha ugaidi wakitafuta fursa za kiuchumi na kisiasa ndio unaoelezwa na baadhi ya wachambuzi kuwa umelenga kudhoofisha amani ambayo Tanzania imedumu nayo kwa miaka mingi ili pale itakapovurugika rasilimali zake lukuki kama dhahabu, mafuta na gesi ziweze kuchumwa kwa urahisi. 

Mkakati huo ndio unaodaiwa kuleta msukumo wa mataifa kutaka Mahakama ndogo ya Kimataifa ya Uhalifu ya (ICC) iwepo mkoani Arusha, hapa nchini kwa ajili ya kuamua kesi za kijinai ikiwemo za wapiganaji wa kikundi cha Alshabab na maharamia wa Kisomali wanaodaiwa kuwa ni tishio katika Pwani ya Bahari Hindi, Ukanda wa Afrika Mashariki.

Baadhi ya wafuatiliaji wa mambo waliozungumza na gazeti hili, wanachambua hatua hiyo imechochea kwa kiwango kikubwa na kuifanya Tanzania kuwa katikati ya wimbi la tishio la ugaidi.

Ni kwa muktadha huo wafuatiliaji hao wanasema ndio umeifanya nchi kujijengea maadui na vikundi ama watu ambao wanashitakiwa katika ardhi ya Tanzania kwa kivuli hicho cha ugaidi.

Wakati likiibuka tukio la Arusha la bomu kurushwa kanisani, zipo taarifa nyingine zinazo eleza kuwa kitendo cha nchi za Umoja wa Mataifa (UN) kuitaka Tanzania iyatumie majeshi yake kwenye operesheni za kulinda amani (Peace Keeping) katika nchi zenye migogoro, nayo inaelezwa kuchangia kwa hatari hiyo ya tishio la ugaidi.

Kitendo cha Tanzania kukubali kupeleka majeshi yake kwenda kulinda amani nchini Kongo kupambana na kikundi cha waasi wa M23 ambao tayari walikwisha ionya kuwa isithubutu kufanya hivyo kunauweka usalama wa nchi hatarini na katika kitendawili kigumu hasa kwa wakati huu ambako tayari vimeshuhudiwa vitendo vya kigaidi. 

Tayari M23 wametoa onyo kwa kuandika barua inayosomeka kuwa wasilaumiwe kama raia wa Tanzania watapatwa na mauaji ya halaiki endapo Serikali itaendelea kupeleka askari wake kujiunga na mpango wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Kongo.

Hivi karibuni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe alikiri kuiona barua hiyo, aliyosema kuwa ilielekezwa kwake pamoja na Bunge hata hivyo Waziri huyo alisema kuwa vitisho hivyo vinatokana na majeshi ya Tanzania kuogopeka na vikosi hivyo vya M23.

Mbali na hilo la M23, uhalifu unaodaiwa kufanywa kwa misingi ya udini nao unaelezwa kuwa ni mkakati unaotekelezwa na mataifa hayo kupitia kwa wanasiasa kwa nia ya kuwagawa Watanzania ili lengo lao la kutafuta fursa za kiuchumi na kisiasa ziweze kufanikiwa.

Mataifa makubwa ikiwemo Marekani yanashutumiwa kupotosha umma wa kimataifa kwa mwamvuli wa ugaidi lengo likiwa ni kutafuta fursa za kujenga uchumi wake kupitia rasilimali toka katika mataifa machanga yanayochipukia kiuchumi. 


UDHAIFU UDHIBITI WA MIPAKA 
Wakati mataifa ya Ulaya yakishutumiwa kuwa nyuma ya mkakati huo, hata hivyo mipaka ya nchi inaelezwa kuwa wazi kiasi cha kutoa fursa ya wageni kuingia na kutoka jinsi wanavyotaka hali ambayo inaelezwa kuhatarisha usalama wa nchi.

Matukio ya wageni kuingia nchini na kufanya uhalifu na kisha kutokomea, yanazua maswali kuhusu hali ya usalama wa nchi hasa kutokana na eneo la kijiografia la Tanzania jinsi lililivyo.

Hatari inayoonekana kwa wageni wengi kuingia nchini kupitia mipaka iliyo wazi inayotoa mianya ya vietendo vya uhalifu kutekelezwa ni jambo jingine linalohatarisha usalama wa nchi. 

Tayari usalama wa kisiwa kama Ukerewe ambacho kimetenganishwa kwa Ziwa Victoria na nchi za Kenya na Uganda, unatiliwa shaka kutokana na hivi karibuni kudaiwa, raia wa kisomali kuingia kinyemela na hivyo kuzua hofu ya ugaidi.

Mbali na Ukerewe maeneo mengine ya mipaka katika maeneo ya Mikoa ya Kigoma ambao umepakana na Kongo, Burundi, Mkoa wa Kagera ambao umepakana na Rwanda na Uganda pia Mkoa wa Rukwa ambao umepakana na Kongo.

Mkoa mwingine ni Mbeya ambao umepakana na nchi ya Zambia na Malawi ambayo katika siku za hivi karibuni imekuwa na mgogoro wa Ziwa Nyasa na Tanzania.

Baadhi wanaohoji juu ya hilo wanakumbushia jinsi nchi hiyo Marekani walipotosha umma wa kimataifa wakitafuta fursa za kiuchumi na kisiasa nchi zilizopinga sera zake mf. Sadam Hussein (Iraq) but wauaji wa Rais John Kennedy hawakuita magaidi.

Kwao kikundi cha LRA cha Joseph Kony ni haramu lakini waasi wa Libya na Syria ni wazalendo. Watawala wetu wameiga hayo ili watu waogope kuwapinga.Waliomdhuru Padre Ambrose Nkenda au Dr.Ulimboka, waliomuua Padre Evarist Mushi, RPC Barlow, Prof.Mwaikusa

0 comments:

Post a Comment