WANAWAKE WAFURIKA KUPATA HUDUMA
BIASHARA
huria imezua mengi. Hali kadhalika Sayansi na Tekenolojia nayo,
imeleta mengi. Katika kuwaondolea kero wanawake wenye matiti
yaliyosinyaa hapa nchini, wataalamu kutoka China wameanza kutoa huduma
ya kunyanyua
matiti hayo kwa kutumia mashine maalumu.
Wachina
wamejipatia umaarufu katika kuleta bidhaa mbalimbali hapa nchini,
zikiwamo za kuongeza nguvu za kiume, kupunguza uzito, kuotesha nywele,
kujichubua (kumfanya mtu mweusi awe mweupe), kuongeza makalio nk.
Huduma
hiyo ya kusimamisha matiti yaliyolala, imeanza kutolewa katika Saluni
ya Blue Palace, iliyopo nyuma ya Shule ya Mapambano, Sinza jijini Dar
es Salaam.
Haikuwa
rahisi kuweza kuamini kuwa vitu kama hivi vinaweza kupatikana
Tanzania. Mwananchi Jumapili lilifunga safari mpaka kwenye saluni hiyo
inayomilikiwa na Sarafina Mtweve, kujionea jinsi teknolojia hiyo
inavyofanya kazi.
Mbali
na meneja wa saluni hiyo, Trust Mwembe, pia alikuwepo mtaalamu kutoka
China aitwaye, Ciisy Pang, ni binti wa miaka 23 tu, lakini anasema kwa
miaka minne amefanya kazi hiyo na kuwasaidia wanawake mbalimbali
waliokuwa wakikerwa na matiti yaliyolegea au kuanguka.
Pang
na kundi lake wanatoa huduma hii kwa gharama ya Sh150,000 kwa kuanzia,
ingawa wanahisi gharama hizo zitapanda katika siku chache zijazo.
Jinsi matiti yanavyosimamishwa
Mashine
hiyo inayoitwa ‘Beauty Machine’ ina uwezo wa kusimamisha matiti ya
kila saizi kwa kuwa huambatanishwa na vibakuli (cups) kama unavyoona
pichani.
Kazi kubwa ya mashine hiyo ni kuamsha misuli ambayo hushikilia nyama za matiti.
Pang
anasema, zoezi la kusimamisha matiti huchukua wiki tatu mpaka sita,
inategemea aina ya mteja na wakati mwingine juhudi zake.
Mtaalamu
huyo ambaye anazungumza Kichina na kutafsiriwa na meneja wa saluni
hiyo, anaelezea namna anavyofanya kazi ya kuyarudisha matiti kwa muda
huo.
“Kwanza
unapaswa ujue kuwa hatutumii dawa yoyote katika zoezi hili, mteja wetu
akifika hapa, kinachotumika ni mashine tu ambayo hutumia umeme kama
zilivyo dryer za nywele,
“Baada
ya kumlaza katika kitanda kile, tunachukua kitu mfano wa bakuli (cups)
mbili kulingana na ukubwa wa matiti yake, tunayatumbukiza humo, kisha
tunawasha mashine,” anasema Pang.
Mtaalamu
huyo anasema mashine hiyo ikiwashwa inavuta kama ‘vacuum’, na inaweza
kuongezwa kasi au kupunguzwa kama inavyofanyika kwenye mashine za
kufanyia mazoezi.
“Tunaiwasha
mashine kwa muda wa dakika 45, mteja atachagua siku mbili katika wiki
za kufanya zoezi hili mpaka litakapokamilika,”anasema Pang.
Tangu
mashine hiyo iwasili nchini, takribani mwezi mmoja uliopita, Pang
anasema ana wateja wanane anaowahudumia kwa nyakati tofauti ambao
wamekiri kuwa maendeleo yanatia moyo.
Ni kweli mashine hii inasaidia?
Akizungumza
kwa njia ya simu, mmoja wa wateja anayepata huduma hiyo ambaye
alijitambulisha kwa jina moja tu Irene anasema, ni wiki ya tatu sasa
tangu aanze kupata huduma hiyo, anakiri kuwa matiti yake sasa yameanza
kuwa magumu tofauti na mwanzo.
“Kusema
kweli nilikuwa na matiti yaliyosinyaa wala si kulala tu kama
ulivyouliza, ila naona sasa yameanza kuwa magumu na kurudi juu kidogo,”
anasema Irene.
Akizungumzia
ugumu anaoupata katika zoezi hilo, anasema safari za kila wiki saluni
na zile dakika 45 za kukaa kwenye mashine zinamchosha, lakini kwa kuwa
amedhamiria, amejitoa mpaka zoezi hilo litakapokamilika.
Matiti yanaweza kulegea tena?
Pang
anasema kama matiti yanalegea kwa sababu fulani mfano uzazi wa watoto
wengi, basi yanaweza kulegea tena kama mtu atajifungua na kunyonyesha
kwa muda huo.Aidha anasema wanawake wenye matiti makubwa, ni rahisi
kuanguka kama hawatayavalisha sidiria kwa muda mrefu.
“Wanawake
wenye matiti makubwa huwa nawashauri kuvaa sidiria hasa wakati wa
mchana na usiku wanaweza kuacha kuzivaa, hii inasaidia kuimarisha
misuli inayoyabeba matiti,” anasema Pang.
Jamii inazungumziaje jambo hili
Baada
ya kusikia kuwepo kwa mashine hii nchini, wanawake mbalimbali wamesema
wanatamani kupata huduma hiyo lakini wengine, walionyesha woga juu ya
matokeo yake.
“Ni
kweli baada ya kunyonyesha watoto wawili sasa matiti yamelegea kabisa,
natamani yarudi kama wakati ule wa usichana wangu, lakini nahofia
huenda mbele ya safari nikapata madhara,” anasema Linda Masatu.
Linda
anaongeza kusema kuwa ni vizuri mwanamke akawa na matiti yaliyojaa
vizuri, lakini anahofia njia zinaweza kuwa na madhara, huku akisema
kama ingetokea njia nyingine ya asili asingesita kuifuata.
Naye
Batuli Famau, anasema mwanamke anapokuwa na matiti yaliyosinyaa mvuto
wake hupungua, hata anapovaa sidiria anakuwa amebadili mwonekano wa nje
tu, lakini ndani bado anakuwa vilevile.
“Mwanamke
mrembo ni yule mwenye matiti mazuri, sasa inapobidi kutumia njia
fulani ili yarudi kama tulipokuwa vigoli, tutafanya tu ili mradi kama
njia hizo hazitatuangamiza,” anasema
Wanaume nao wameonekana kuunga mkono zoezi la kusimamisha matiti ingawa wengine hawaungi mkono utumiaji wa mashine hii.
Augustino
Magara anasema: “Ni kweli mwanamke mwenye matiti magumu anavutia
kuliko yaliolegea na kulala, lakini sasa tuwe makini kabla wake zetu
hawajaumia katika mashine, hizi”
“Wote
tunajua sababu zilizosababisha matiti ya wake zetu yalegee, sioni
sababu ya kusema tunataka yaliyo magumu, tuwapende wake zetu hivi hivi
na tuwape moyo,” anasema Nganara.
Dk
Innocent Mosha wa Kitengo cha Patholojia Hospitali ya Taifa ya
Muhimbili, anasema ni vigumu kwa wataalamu wa afya kugundua madhara ya
mashine hizo kwa haraka hadi pale uchunguzi utakapofanyika.
“Ingelikuwa
mazoezi hayo yanachukua muda mfupi, kweli tungepata wasiwasi kwa kuwa,
unapoisimamisha misuli kwa haraka ni lazima madhara yatokee, lakini
hili la mazoezi, bado sifahamu,” anasema Dk Mosha.
DUUUUUUUUUH, WANAWAKE...... KAZI KWELI KWELI.....
MUNGU ATUNUSURU
0 comments:
Post a Comment