Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willbrod Slaa akiongozana na viongozi wa
Umoja wa Wanafunzi wa Vyuo Vikuu wa Chama hicho (CHASO) wakati wa
ufunguzi wa Kongamano la wanafunzi wa vyuo vikuu lililofanyika katika
Ukumbi wa Msimbazi jijini Dar es Salaam jana. Picha na Fidelis Felix
Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willbroad Slaa amesema kuwa kuanzia
mwaka huu hadi 2015, chama chake kitaipeleka mchakamchaka CCM, kwa kuwa
chama chake kimefanikiwa kuwaamsha Watanzania.
Alisema
kwamba Watanzania sasa wameamka na kutambua utajiri wa nchi yao na
jinsi rasilimali zinavyotoroshwa nje ya nchi na kuanza kudai
kufaidika nazo kwa nguvu. Hivyo Chadema kitaitumia fursa hiyo kuipeleka
puta CCM, lengo likiwa kuhakikisha kila Mtanzania anaishi maisha bora.
Dk
Slaa alisema hayo alipokuwa akizungumza katika kongamano la Umoja wa
Wanafunzi wa Vyuo Vikuu nchini, ambao ni wafuasi wa chama hicho
(CHASO), lililofanyika Dar es Salaam jana.
Alieleza
kuwa kinachotokea mikoa ya Lindi na Mtwara, pamoja na maandamano ya
hivi karibuni ya wanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) ni
majibu tosha kwa CCM, kwamba mikutano ya Chadema iliyofanyika mikoa
mbalimbali nchini imewaamsha wananchi.
Wanafunzi
zaidi ya 500 walihudhuria kongamano hilo kutoka IFM, Chuo Kikuu Dar es
Salaam (UDSM), Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Chuo Kikuu cha
Kimataifa cha Kampala (KIU), Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu (DUCE) na
Chuo cha Teknolojia Dar es Salaam (DIT), pamoja na vyuo mbalimbali
vilivyopo Dar es Salaam na mikoani.
Desemba
18 mwaka jana Mwenyekiti wa Chama hicho, Freeman Mbowe alisema kuwa
mwaka huu utakuwa ni wa kuunganisha nguvu ya umma kitaifa, baada ya
Serikali ya Rais Jakaya Kikwete kushindwa kuzifanyia kazi hoja
mbalimbali zinazotolewa na chama hicho.
Dk
Slaa ambaye alitumia saa 1:06 kuzungumza na wanafunzi hao, alisema kuwa
elimu ya uraia waliyoitoa kwa wananchi katika mikutano ya Vuguvugu la
Mabadiliko (M4C), pamoja na Operesheni Sangara, wamefanikiwa kwa
asilimia 99.
“Tumewapa
elimu ya uraia wananchi katika mikoa yote nchini na sasa wanajua haki
zao,.Hiyo ni kazi na mikutano yetu pamoja na maandamano tuliyoyafanya”
alisema Dk Slaa na kuongeza:
“Nawapongeza
wanafunzi wa IFM kwa kuandamana, najua wapo watakaosema nachochea
maandamano, lakini wanatakiwa kujua kwamba wanafunzi hawa walikuwa na
haki, haiwezekani wanabakwa kisha wakae kimya, tena wametoa taarifa
polisi na hakuna kilichofanyika.”
Mbali
na kutaka Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Said Mwema na Kamanda wa
Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova kujiuzulu kwa
kitendo cha kuamuru wanafunzi wa IFM kupigwa wakati walikuwa wakililia
usalama wao, alisema kwamba kuna tofauti kubwa kati ya vurugu na kudai
haki za msingi.
“Inakuwaje
polisi wanawapiga mabomu wanafunzi wanaofanya maandamano, lakini
wanashindwa kuzuia Twiga wanaotoroshwa nje ya nchi, tuungane,
tushirikiane na tupige kelele, ili mali zetu zirudi,” alisema Dk Slaa
na kuongeza:
“Wananchi wa Mtwara na Lindi sasa wanaandamana kutaka gesi iwanufaishe wao kwanza.
0 comments:
Post a Comment