mkuu wa wilaya ya Arusha, John Mongela alipokuwa akiongea na waandishiwa habari juu ya mafanikio ya chama cha mapinduzi (CCM) kwa miaka 7 (kuanzia mwaka 2005 hadi desemba 2012) |
Imeelezwa kuwa ilani ya ccm kwa miaka saba katika wilaya ya
arusha imefanikiwa kwa kiasi kikubwa katika njanja zote zikiwemo sector ya
elimu ,afya,mazingira,na miundombinu ikiwemo mji wa Arusha kutoka manispaa hadi
kuwa jiji rasmi.
Hayo yameelezwa na mkuu wa wilaya ya arusha john Mogella
mbele ya waandishi wa habari wakati akitoa taarifa hiyo ambapo amesema kuwa
sector zote zimefanikiwa kwa kiasi kikubwa kwani toka mwaka 2005 hadi mwaka desemba
2012 karibu ahadi zote za ilani ya chama cha mapinduzi zimetekelezwa.
Bw Mogella amesema katika sector ya elimu wamejenga madarasa
172na matundu ya vyoo 225,ambapo shule za msingi zimeongezeka 70 ambapo kwa
shule za sekondari zimeongezeka 23 huku awali zilikuwa saba ,pia walimu na
vifaa vya usimamizi wameongezeka ikiwemo walim kuajiriwa 534 kwa miaka hiyo
saba pamoja na idadi ya vyuo vya shahada ya juu vilivyopandishwa hadhi na kuwa vtuo vikuu kufikia 8 .
Kwa upande wa afya mongela amesema kuwa wameweza kuboresha
huduma ya mama na mtoto ambapo vituo 5 na zahanati 68 zimeboreshwa kwa uhakika
wa upatikanaji wa dawa na huduma bora, huku akifafanua kuwa wameipandisha hadhi
kituo cha afya cha kanisa la st.elizabert na kuwa hospitali ya wilaya huku akisema
kuwa katika hospitali hiyo kuna kituo kikuu kitakachotoa huduma kwa watu
wanaoishi na virusi vya ukimwi ambapo wahusika watahudumiwa bure.
Kwa upande wa miundo mbinu amesema kuwa barabara nyingi
zimejengwa kwa kiwango cha lami hasa za katikati ya mji ambapo hadi sasa
barabara 23 zenye urefu wa km 8 zimekamilika ambapo mradi huu unaofadhiliwa na
benki ya dunia kwa kiasi cha dola million 7 za kimarekani,ikiwa ni kwa awamu ya
kwanza na awamu ya pili itajenga barabara ya njiro,kanali ndomba,pamoja na kujenga
dampo la kisasa ,sambamba na ujenzi wa madaraja 9 katika wilaya ya arusha.
Akiongelea upande wa mazingira hasa katika maji safi na taka amesema asilimia 83 ya
wakazi wanaoishi katika jiji la arusha wanapata maji safi na salama tofauti na
awali ilikuwa ni asilimia 42 tu ya wakazi ndio waliokuwa wanapata huduma hiyo
ya maji salama ,ambapo amesema kuwa wanamkakati wa kuboresha miundo mbinu ya
maji safi na taka utakao gharimu takribani shilingi million moja.
Katika swala la mazingira amesema wamepiga hatua kwani
wameweza kulinda vyanzo vya maji kwa kushirikiana na AUWSA ikiwemo
misitu,kuzuia uoshaji wa magari pembezoni mwa vyanzo vya maji na mito pia kuzuia
ukataji wa miti katika misitu na kujenga kwenye vyanzo iliyopo ndani ya jiji na
sasa nguvu kubwa wanaboresha usafi ndani ya jiji letu.
Aidha alisema pamoja na mafanikio hayo pia kuna changamoto
zinzoikabili jiji hili ikiwemo ya kusafisha hati chafu ya jiji hili ,ambapo
baadhi ya viongozi wabadhirifu wa raslimali wamewajibishwa kutokana na makosa yao ikiwemo kufikishwa
mahakamani paoja na kufukuzwa kazi.
Pia aliongezea kuwa changamoto nyingine ni demokrasia ambapo
wilaya yetu ina viongozi wa vyama vya
siasa tofauti tofauti ambapo alitolea mfano mbunge wa chadema katika jimbo la
mjini arusha kutofautiana katika utekelezaji na uwajibikaji katika kuwatumikia
wananchi wa wilaya hii .
Mwisho mkuu wa wilaya ya arusha Mogella alitoa wito kwa
wakazi wa jiji la arusha kuendelea kushirikiana na viongozi katika kuhakikisha
hali ya jiji inakuwa tulivu ambapo kwa kiasi kikubwa katika swala la ulinzi na
usalama ikiwemo dhana ya ulinzi shirikishi na tii sheria bila shuruti
imefanikiwa kwa kiasi kikubwa.
baadhi ya waandishi wa habri wakisikiliza kwa makini mkuu wa wilaya
0 comments:
Post a Comment