Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mh.Nyirembe Munassa akifungua mkutano.
Imeelezwa kuwa kukuwa
kwa uchumi duniani hasa kwa nchi zinazo endelea kunategemea njia bora
za utunzaji wa mazingira kwa kuzingatia uzalishaji bora wa viwanda
unaoendana na viwango vya kimataifa
Hayo yameelezwa
jijini Arusha leo wakati wa mkutano wa viongozi wa kimataifa
wanaoshughulikia viwango vya maswala ya mazingira duniani,ambapo mgeni
rasmi katika mkutano huo alikuwa mkuu wa wilaya ya Arumeru Mh.Nyirembe
Munassa
Nyirembe Munassa
amesema nchi za dunia ya tatu ziko katika hali mbaya zaidi kutokana na
uwezo duni wa kupambana na athari za mabadiriko ya tabia nchi
Nae mwenyekiti wa
mkutano huo Prof. Robert Page amesisitiza kuanzishwa kwa mkakati
madhubuti wa kupunguza athari hizo kutokana na kwamba maendeleo ya
kiuchumi yoyote hutegemea kwa kiasi kikubwa mazingira yaliyo tunzwa
vizuri
Mkutano huo ni wa
siku mbili unaoshirikisha wataalamu wa viwango na wadau wa mazingira
duniani, pamoja na mambo mengine utajadili mpango wa kuwa na
teknolojia safi katika uzalishaji wa bidhaa mbalimbali duniani kote
0 comments:
Post a Comment