NA MOHAMEDI ISIMBULA -DONGOBESHI
Imeelezwa kuwa kukwama kwa wanafunzi wa kidato
cha kwanza kuanza masomo yao
katika shule ya sekondari ya Alexander Saulo iliyoko Dongobeshi wilayani mbulu
kunachangiwa na siasa chafu zinazofanywa na wanasiasa katika kata hiyo
Akitoa taarifa hiyo kwa mkuu wa wilaya hiyo
Anatori Choyo aliyetembelea shule hiyo na kufanya kikao na kamati ya maendeleo
ya kata hiyo mwenykiti wa bodi ya shule hiyo Yoramu Gefi alimweleza mkuu huyo
kuwa wanasiasa ndiyo chanzo kikubwa cha ujenzi wa vyumba hivyo kukwama
Aidha alisema katika hali hiyo isiyokuwa ya
kawaida baadhi ya wanasiasa kupitia vyama viwili ambavyo vinaonekana kuwa na
nguvu katika kata hiyo ni Chadema na CCM ambapo viongozi wake wamekuwa
wakiwashawishi wanananchi kutoshiriki katika kazi ya ujenzi wa vyumba hivyo vya
shule hiyo ili kuwawezesha wanafunzi hao kuanza masomo yao mapema
Katika taarifa yake hiyo alisema jumla ya vyumba
vya madarasa vitano vinahitajika katika shule hiyo hali ambayo bado ni tete
kutokana gubiko hilo la kisiasa kuendelea
kuikumba kata hiyo na kusababisha wananchi wake kusahau wajibu wao katika
maendeleo yao
Naye mkuu wa wilaya hiyo mara baada ya kupokea
taarifa hiyo aliwataka viongozi wa vyama hivyo kuacha siasa hizo na badala yake
wawahamasishe wananchi kushiriki katika kazi za ujenzi wa shule hiyo ili watoto
wao waweze kuanza masomo yao
mapema
Mkuu huyo pia alisema siyo vyema wanafunzi hao
wakaendelea kuteseka kwa masuala kisiasa na hasa ukizingatia kuwa muda wa
malumbano ya kisiasa bado haujafika
,,ndugu zanguni nawaombeni kama
mna mambo yenu ya kisiasa yacheni kwanza tuangalie watoto wetu tuliwasomesha
sisi wenyewe katika shule za misingi halafu leo tunawasusia kuwajengea
shule za sekondari hivi jamii itatueleweje alihoji mkuu huyo
Pia alisema kutokana na kikao hicho ambacho
kimekaa na kuona tatizo hilo yeye kama mkuu wa wilaya hiyo kwa kushirikana na
idara ya elimu sekondari mbulu atendesha zoezi hilo la ujenzi wa vyumba
hivyo na kuhakikisha wanafunzi hao wanaanza masomo yao
“siwezi kukubali fedheha hii ya wanafunzi
waliyofaulu vizuuri wakae nyumbani eti kosa hakuna vyumba vya madarasa hilo halitawezekana
hata kwa kukamatana nitahakikisha wanafunzi hao wote wanakwenda shule na si
vinginevyo” alisema choya
Charles Sulle ni mkuu wa shule naye alimweleza
mkuu huyo kuwa hana chumba hata kimoja cha kuwaweka wanafunzi hao jambo
linalomfanya ashindwa kutoa elimu kwa wanafunzi hao wanadaiwa kuchelewa zaidi
ya mwezi baada ya shule kufunguliwa.
0 comments:
Post a Comment