Desemba 31: Kesi ya Ponda kuendelea leo
Shahidi wa nne wa upande wa Jamhuri katika kesi ya uchochezi na wizi wa Sh milioni 59 inayomkabili Katibu wa Taasisi na Jumuiya na Taasisi za Kiislamu(T), Sheikh Issa Ponda na wafuasi wake 49 leo anatarajia kuanza kupanda kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuanza kutoa ushahidi wake.
Desemba 28: Korti Kuu yaipa namba kesi ya Lulu
Hatimaye uongozi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, umeipatia namba jarada la kesi ya mauji ya bila kukusudia inayomkbaili msanii wa filamu nchini Elizabeth Michael maarufu kama ‘Lulu’.
Desemba 27: Upelelezi kesi ya Papa Msoffe bado
Upande wa Jamhuri katika kesi ya mauaji inayomkabili mfanyabiashara maarufu jijini Dar es Salaam, Marijani Abdubakari Msoffe(50) maarufu kwa jina la “Papa Msoffe chuma cha reli akishiki kutu’ ’
jana umeieleza tena Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa upelelezi wa
kesi hiyo bado haujakamilika na Hakimu Agnes Mchome akaiarisha kesi hiyo
hadi Januari 9 mwaka huu,itakapokuja kwaajili ya kutajwa.
Desemba 24; Mahakama Kuu yamnyima dhamana Hassanor
Jaji wa Mahakama Kuu Zainabu Mruke ametupilia mbali ombi la Mwenyekiti wa Chama
Cha Soka Mkoa wa Pwani(COREFA), Hassan Othman Hassan ‘Hassanoo’
lilokuwa likiomba mahakama impatie dhamana.Jaji Mruke alisema mahakama
yake imefikia uamuzi wa kumnyima dhamana Hassanoor ambaye kwasasa
anakabiliwa na kesi ya Sh. bilioni 1.1 kwa kusafirisha pembe za ndovu toka Tanzania kwenda Hong Kong nchini China.
Jaji
Mruke alisema anamnyima dhamana kwasababu yupo nje kwa dhamana ya kesi
Na.209/2011 ya wizi wa Shaba zenye thamani ya milioni 400 na wakati yupo
nje ya dhamana ya kesi hiyo amefunguliwa kesi nyingine ya usafirishaji
wa pembe za ndovu.
Desemba 21: Godbles Lema arejeshewa ubunge wake
Mahakama
ya Rufaa Tanzania, imetengua hukumu iliyotolewa na Mahakama Kuu Kanda
ya Arusha ,Aprili 15 mwaka huu, iliyokuwa imemvua ubunge Mbunge wa Jimbo
la Arusha Mjini(Chadema), Godbles Lema, kwasababu imebaini hukumu ile
ilikuwa na mapungu ya kisheria.
Desemba 21: Kesi ya Lulu yaamishiwa Mahakama Kuu:
Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, uliifunga rasmi kesi ya kuua bila kukusudia inayomkabili msanii wa filamu nchini
Elizabeth Michael maarufu kama Lulu ambaye anadaiwa kumuua bila
kukusudia msanii mwenzake Steven Kanumba,baada ya upande wa jamhuri
kumaliza kumsomea kwa mapana shtaka linalomkabili mshtakiwa
huyo(Comittal Procedings), ambapo hakimu huyo alisema hatua hiyo ya
upande wa jamhuri kumsomea maelezo hayo kumeifanya mahakaa ya Kisutu
kuifunga kesi hiyo na kuiamishia mahakama kuu kwaajili ya kesi hiyo
kuanza kusikilizwa kwasababu mahakama kuuu ndiyo yenye mamlaka ya
kuisikiliza kesi hiyo na akaamuru Lulu
arudishwe gerezani hadi pale mshtakiwa huyo atakapokea wito wa Mahakama
Kuu.
Desemba 21: Mahakama Kuu yasikiliza ombi la Hassanor
Jaji Zainabu Mruke wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, alisikiliza ombi la dhamana lilowasilishwa mbele yake ya Mwenyekiti
wa Chama Cha Soka Mkoa wa Pwani(COREFA), Hassan Othman Hassan
‘Hassanoo’ na wenzake sita wamaokabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi wa Sh
bilioni 1.1 kwa kusafirisha pembe za ndovu toka Tanzania kwenda Hong
Kong nchini China.
Desemba 20;Hakimu akwamisha kesi ya Vigogo Suma JKT
Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu , Alocye Katema ameshindwa kutokea
mahakamani kwa sababu alikuwa na udhuru na kusababisha shahidi wa
kwanza wa upande wa jamhuri katika kesi ya matumuzi mabaya ya madaraka
inayomkabili Mkurugenzi wa Shirika la Kujenga Taifa (SUMA JKT), Kanali
Ayoub Mwakang’ata na maofisa wengine wa jeshi hilo kushindwa kuanza
kutoa ushahidi wake.
Desemba 18:Sangoma anaswa na matunguli mahakama ya Kisutu
Kifaa
maalumu kinachotumiwa na wanausalama kuwapekua watu wanaoingia kwenye
eneo la Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, siku ya kesi ya uchochezi
na wizi wa Sh milioni 59 inayomkabili Katibu wa Jumuiya na Taasisi za
Kiislamu nchini, Sheikh Ponda Issa Ponda na wenzake 49 inapokuja
kusikilizwa mahakamani hapo, kimefanikiwa kumnasa mganga wa kienyeji
Rajabu Zuberi(30) akiwa na vifaa vyake vya kiganga ‘ matunguli’ ambaye
alikuja kufanya mambo ya kishirikina mahakamani hapo ambayo yangeweza
kumsaidia mteja wake anayekabiliwa na kesi ya jinai mahakamani.
Desemba 17: Jaji Mkuu awataka mawakili wajikite vijijini
Jaji
Mkuu wa Tanzania Mohamed Chande Othman amewataka wamawakili
wakujitegemea wapya waende kutoa huduma ya sheria vijijini kwani huko
vijijini kuna wananchi wanaoitaji huduma hiyo.
Wito
huo ulitolewa leo na Jaji Othman katika sherehe ya 47 ya kuwakubali na
kuwasajili mawakili wapya 618 katika viwanja vya Shule ya Sheria
Tanzania iliyopo Sinza ‘C’ jijini Dar es Salaam, ambapo alisema hata
huko mikoani kuna mahakama pia ambapo wananchi wanataka kuwakilishwa na
mawakili wa kujitegemea mahakamani.
Desemba 18: Sheikh Ponda mgonjwa.
Katibu
wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini, Sheikh Ponda Issa Ponda na
wenzake 49 ambaye wanakabiliwa na kesi ya uchochezi na wizi wa malighafi
zenye thamani ya Sh 59,wakili Mwandamizi wa Serikali Tumaini Kweka
alisema kesi hiyo ilikuja kwaajili ya kutajwa na kuendelea kusikilizwa
lakini amepokea taarifa toka kwa maofisa wa Jeshi la Magereza kuwa Ponda
anayeishi katika gereza la Segerea ni mgonjwa hivyo wameshindwa kumleta
mahakamani.
Desemba 11:Mahakama ya Rufaa yakwamisha Rufaa ya DPP v Zombe
Mahakama
ya Rufaa nchini jana ilishindwa kuanza kusikiliza rufaa iliyokatwa na
Mkurugenzi wa Mashtaka(DPP), Dk.Eliezer Feleshi dhidi ya aliyekuwa Mkuu
wa Upelelezi wa Mkoa wa Dar es Salaam (ACP), Abdallah Zombe na wenzake
kwa sababu jaji mmoja Semistockles Kaijage anayeunda jopo la majaji
watatu anaumwa.
Desemba 7: Chadema yailiza CCM Ubungo
Mahakama
ya Rufani jijini Dar es Salaam, imetoa amri ya kuiondoa rufaa iliyokuwa
imekatwa na aliyekuwa mgombea ubunge wa jimbo la Ubungo(CCM), Hawa
Ng’umbi dhidi ya Mbunge wa Jimbo la Ubungo(Chadema) na wenzake bila
gharama baada ya kuridhia maombi ya pande zote mbili zilizokuwa
zimeiomba mahakama hiyo iiondoe rufaa hiyo mahakamani.
Desemba 4:Lema atoa sababu 18 kutetea ubunge wake
Aliyekuwa
mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini(Chadema),Godbles Lema ,amewasilisha
sababu 18, kuiomba Mahakama ya Rufaa nchini, itengue hukumu ya mahakama
kuu Kanda ya Arusha iliyolewa Aprili 15 mwaka, ambapo ilitengua ubunge
wake. yotolewa
na Mahakama Kuu Kanda ya Arusha Aprili mwaka huu ambayo ilitengua
ubunge wake.yotolewa na Mahakama Kuu Kanda ya Arusha Aprili mwaka huu
ambayo ilitengua ubunge wake.
Novemba 29: Katibu Bakwata amruka Ponda
Katibu Mkuu wa Baraza la Kuu la Waislamu(BAKWATA), Suleman Said Lolila(61),amekanusha madai yaliyotolewa na Katibu
wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini, Sheikh Ponda Issa Ponda na
wenzake 49 wanaokabiliwa na kesi uchochezi na wizi wa Sh milioni 59
katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, kuwa Baraza Kuu la
Waislamu nchini(BAKWATA), siyo chombo cha kuwakilisha waislamu wote
hapa nchini.
Suleiman
ambaye ni shahidi wa kwanza wa upande wa jamhuri katika kesi hiyo,
alitoa maelezo hayo jana mbele ya Hakimu Mkazi Victoria Nongwa wakati
akiongozwa na wakili mwandamizi wa serikali Tumaini Kweka kumuongoza
kutoa ushahidi ambapo jana shahidi huyo alimaliza kutoa ushahidi wake.
Novemba 28: Hatiwa atiani kwa makosa ya kufanyabiashara haramu ya kusafirisha binadamu
Mahakama
ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam,imemtia hatiani mfanyabiashara wa
ngozi nchini, Salim Ally (61) kwa makosa ya kusafirisha binadamu na
kuwatumisha na kumhukumu kwenda jela miaka 10 au kulipa fidia ya jumla
ya milioni 17.
Hukumu
hiyo ya kesi hiyo ya ki historia na ya kwanza kutolewa katika Mahakama
hiyo tangu Sheria ya Usafirishaji haramu binadamu ya mwaka 2008
ilipotungwa na bunge, ilitolewa na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo
Ilvin Mugeta.
Novemba 28:Mahakama yambwaga Hamad Rashid
Mahakama
Kuu Kanda ya Dar es Salaam imetupilia mbali ombi lilotaka mahakama hiyo
itoe amri ya kuliita Baraza la Wadhamini wa Chama cha Wananchi(CUF) na
wenzake waje wajieleze ni kwanini walikaidi amri ya mahakama na ni
kwanini wasitiwe hatiani kwa kosa la kudharau amari ya mahakama ambalo
liliwasilishwa mahakamani hapo na Mbunge wa Wawi(CUF), Hamad Rashid na
wenzake 10.
Rashid na wenzake waliwasilisha maombi mahakamani hapo Januari 10, 2012,na walikuwa wakiiomba mahakama iwaite Wadhamini
wa Cuf wajieleze ni kwa nini wasitiwe hatiani kwa kukiuka amri ya
mahakama hiyo kutokana na uamuzi wa Baraza la Taifa la Uongozi la Cuf
kumfukuza uanachama Hamad na wenzake.
Novemba 23:Maranda,Farijala wahukumiwa tena
Mahakama
ya Hakimu Mkazi Kisutu , imemhukumu kwenda jela miaka miwili kada wa
Chama cha Mapinduzi (CCM), Rajabu Maranda, na wenzake waliokuwa
wakikabiliwa na kesi ya kughushi na kuisababishia serikali hasara ya sh
bilioni 3.8 katika Akaunti ya Madeni ya Nje katika Benki Kuu ya Tanzania
(EPA) .
Novemba 27: Hassanor sasa akimbili Mahakama Kuu
Mwenyekiti
wa Chama cha Soka mkoa wa Pwani (Corefa), Hassani Othman maarufu kama
Hasanoo (43) na wenzake watano ambao wanakabiliwa na mashtaka matatu
likiwemo kosa la uhujumu uchumi na kusafirisha Pembe za ndovu zenye
thamani ya Sh.bilioni 1.1 kwenda Hong Kong nchini China, katika Mahakama
ya Hakimu Mkazi Kisutu, amewasilisha ombi la kuomba apatiwe dhamana na
Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.
Novemba 23 mwaka huu ; Pembe za ndovu zamfikisha mahakamani Hassanor
Mwenyekiti
wa Chama cha Soka mkoa wa Pwani (Corefa), Hassani Othman maarufu kama
Hasanoo (43) na wenzake watano wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu
Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka matatu likiwemo kosa la uhujumu
uchumi na kusafirisha Pembe za ndovu zenye thamani ya Sh.bilioni 1.1
kwenda Hong Kong nchini China.
Novemba 22: Maranda,Farijala wafungwa tenaMahakama ya Kisutu imemhukumu kwenda jela miaka miwili Kada wa Chama cha Mapinduzi(CCM), Rajabu Maranda,Farijala Hussein na maofisa watatu wa Benki Kuu, waliokuwa wakikabiliwa na makosa kugushi, kuisababishia serikali hasara na wizi wa sh bilioni 3.3 katika akaunti ya EPA.
Novemba 22: Maranda,Farijala wafungwa tenaMahakama ya Kisutu imemhukumu kwenda jela miaka miwili Kada wa Chama cha Mapinduzi(CCM), Rajabu Maranda,Farijala Hussein na maofisa watatu wa Benki Kuu, waliokuwa wakikabiliwa na makosa kugushi, kuisababishia serikali hasara na wizi wa sh bilioni 3.3 katika akaunti ya EPA.
ya
kughushi,na kuisababishia serikali hasara ya Sh.bilioni 3.8 katika
Akaunti ya Madeni ya Nje katika Benki Kuu ya Tanzania .ya kughushi,na
kuisababishia serikali hasara ya Sh.bilioni 3.8 katika Akaunti ya Madeni
ya Nje katika Benki Kuu ya Tanzania .iliwa na kesi ya kughushi,na
kuisababishia serikali hasara ya Sh.bilioni 3.8 katika Akaunti ya Madeni
ya Nje katika Benki Kuu ya Tanzania .
Novemba 20: Askari wa JWTZ waliomua Swetu Fundikira wahukumiwa kifo
Mahakama
Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imewahukumu adhabu ya kunyongwa hadi kufa
askari wawili wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na mmoja wa Jeshi la
Wananchi (JWTZ), baada ya kuwatia hatiani kwa kosa la kumuua kwa
kusudia, Swetu Fundikira.Askari hao MT 1900 Sajenti Roda Robert (42) wa
JKT, Kikosi cha Mbweni, MT 75854 Koplo Ally Ngumbe (37) wa JWTZ, Kikosi
cha Kunduchi na MT 85067 Koplo Mohamed Rashid wa JKT Mbweni.
Oktoba 22: Sheikh Farid aburutwa kortini ,anyimwa dhamana
Mwenyekiti wa Jumuia ya Maimamu Zanzibar Sheikhe Farid hadi Ahmed(41) na wenzake sita wamefikishwa katika Mahakama ya wilaya ya Mwanakwelekwe,Zanzibar wakikabiliwa na makosa ya kufanya mikutano na kupelekea ghasia zilizoleta uvunjifu wa amani na uhalibifu wa miundombinu ya barabara.
Oktoba 19:Korti Kuu yamgomea Dk.Slaa
Hatimaye
Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imetupilia mbali kwa gharama
pingamizi lilowasilishwa mbele yake na Katibu Mkuu wa Chama cha
Demokrasia na Maendeleo(Chadema), Dk.Willbrod Slaa lililokuwa likiomba
mahakama hiyo ifute kesi ya madai iliyofunguliwa na mkewe Rose Kamili
Slaa nee Sakum akiomba mahakama hiyo imzuie mumewe Dk.Slaa asifunge ndoa
na mchumba wake Josephine Mushumbusi.
Oktoba 18: Sheikh Ponda kortini kwa uchochezi, wizi
Sheikh
Issa Ponda na wafuasi wake 49 jana walifikishwa katika Mahakama ya
Kisutu chini ya ulinzi mkali wa wanausalama kwa kosa la uchochezi na
wizi wa malighafi zenye thamani ya Shilingi milioni 59.
Katika
hatua nyingine Mkurugenzi wa Mashitaka(DPP),Dk.Eliezer Feleshi
aliwasilishwa mahakamani hapo hati ya kuzuia Ponda asipewe dhamana chini
ya kifungu cha 84(4) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya mwaka
2002, ambapo kifungu hicho kinampa mamlaka DPP kufunga dhamana kwa
mshtakiwa anayekabiliwa na makosa yanayodhaminika na mahakama inakuwa
imefungwa mikono hivyo mahakama inakuwa haina mamlaka ya kuipinga hati
hiyo ya DPP hadi pale siku DPP atakapojisikia kuiondoa mahakamani hati
hiyo.
Oktoba 15: Shabani Mitanga ashinda kesi
Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imemwachilia huru Rais
wa zamani wa Shirikisho la Ngumi Tanzania (BFT), Alhaji Shabani
Mintanga, baada ya kuona hana kesi ya kujibu katika kesi ya kusafirisha
dawa za kulevya iliyokuwa inamkabili.
Mintanga
alikuwa anakabiliwa na kesi ya kula njama na kusafirisha dawa za
kulevya kilo 4.8, kupeleka nchini Mauritius, ambapo Mwaka 2008
alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, akikabiliwa na kesi
hiyo, kutokana na mashtaka yaliyokuwa yanamkabili kwa kutokuwa na
dhamana kisheria, alikuwa mahabusu miaka yote hiyo.
Oktoba 11:Maofisa elimu kortini kwa wizi
Makaimu
Afisa elimu wa Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam, Clara Nyongeja,
Elizabeth Thomas,Mercy Nyalusi,Simon Pilla na Joseph Kaika wamefikishwa
katika Mahakama ya Kisutu mbele ya Hakimu mkazi Agnes Mchome
wakikabiliwa na makosa ya matumizi mabaya ya madaraka ya kuibia serikali
jumla ya shilingi milioni11.8.
Oktoba 11:Mramba ayasuta mashtaka yake
Waziri
wa fedha wa zamani, Basil Mramba ameendelea kuyasuta mashitaka
yanayomkabili katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, na
kudai kuwa siyo yeye aliyeiarika nchini kampuni ya Alex Stewart,wala
kuiongezea mkataba wa nyongeza kampuni hiyo na wala kuiarifu kuwa
ilikuwa imeteuliwa na serikali ya Tanzania kuwa imeshinda tenda na
kwamba inahitajika kuja kufanyakazi hapa nchini wala kuingia mkataba na
kampuni hiyo.
Mramba
aliyasema hayo mbele ya jopo linaongozwa na Jaji John Utamwa, Sam
Rumanyika na Hakimu Mkazi Saul Kinemela wakati alipokuwa akihojiwa na
wakili wa Waziri wa Nishati na Madini wa zamani, Daniel Yona na Katibu
Mkuu Mstaafu wa Wizara ya Fedha, Gray Mgonja, (Elisa Msuya na Profesa
Leonard Shaidi), baada ya juzi wakili wa Mramba (Peter Swai) kumaliza
kumuongoza mshitakiwa huyo kutoa utetezi wake.
Oktoba 9:Rais Mwinyi apanda kizimbani kutoa ushahidi katika kesi ya kuibiwa Sh.Mil.37
Rais
mstaafu wa awamu ya pili, Ally Hassan Mwinyi amefuata nyayo za Rais wa
awamu ya tatu,Benjamin Mkapa kwa kufika katika Mahakama ya Hakimu MKazi
Kisutu Dar es Salaam, na kupanda kizimbani na kutoa ushahidi katika kesi
za jinai zilizofunguliwa mahakamani hapo na Mkurugenzi wa Mashitaka
nchini(DPP), Dk.Eliezer Feleshi dhidi ya washitakiwa wa kesi hizo za
jinai.
Rais
Mwinyi jana alitua katika mahakama hiyo huku akiongozwa na maofisa
Usalama wa Taifa(TISS) kuja kutoa ushahidi katika kesi ya jinai Na.
201/2012 iliyofunguliwa na upande wa Jamhuri dhidi ya wakala wa Mwinyi
Abdallah Nassoro Mzombe(39),mbele ya Hakimu Mkazi Genivitus Dudu ambapo
mshitakiwa huyo ambaye ni Mfanyabiashara na mkazi wa Kinondoni Mkwajuni
anashitakiwa kwa makosa ya kumuibia Rais Mwinyi Sh. 37,440,000 zikiwa ni
kodi ya pango katika nyumba mbili zinazomilikiwa na rais huyo mstaafu.
Septemba 27:Kesi ya Dk.Mkopi yafika patamu
Upande
wa jamhuri katika kesi ya kudhalau amri ya Mahakama Kuu Divisheni ya
Kazi inayomkabili Rais wa Chama cha Madaktari nchini(MALT), Dk.Namala
Mkopi ulimsomea maelezo ya awali mshitakiwa huyo katika Mahakama ya
Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam
Septemba 25: Mtikila ambwaga Kikwete kortini
Hatimaye
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam ,imemfutia kesi ya
uchochezi ya kuchapisha na kumiliki waraka wa uchochezi dhidi ya Rais
Jakaya Kikwete iliyokuwa ikimkabili Mwenyekiti wa Chama cha
Democratic(DP), Mchungaji Christopher Mtikila badaa ya upande wa jamhuri
kushindwa kuleta ushahidi wa kuthibitisha kesi hiyo.
Hukumu
hiyo ya kesi hiyo ya jinai Na.132/2010 ilitolewa jana mchana na Hakimu
Mfawidhi wa Mahakama hiyo,Elvin Mugeta ambapo alianza kwa kuikumbusha
mahakama hiyo kuwa mshitakiwa huyo alikuwa akikabiliwa na makosa
mawili.Kosa la kwanza ni kusambaza waraka wa uchochezi kinyume na
kifungu cha 32(1),(c) cha Sheria ya Magazeti ya mwaka 2002 na kosa la
pili ni la kumiliki waraka huo wa uchochezi kinyume na kifungu cha 32(2)
cha sheria hiyo.
Oktoba 21:Kesi ya Kibanda yaanza kuunguruma
Shahidi
wa kwanza wa upande wa jamhuri katika kesi ya kuandika na kuchapisha
makala ya uchochezi inayomkabili aliyekuwa Mhariri Mtendaji wa gazeti la
Tanzania Daima,Absalom Kibanda, Mkurugezni
Msaidizi anayesajili Magazeti, Rafael Hokororo (57) ameieleza Mahakama
ya Kisutu kuwa waraka uliondikwa na Mwandishi wa gazeti la Tanzania
Daima, Samson Mwigamba ulikuwa unashawishi askari wagome na wasipokee
amri kutoka kwa wakuu wao.
Oktoba 16: Mtoto aliyekojolea Korani Mbagala kortini
Mtoto(jina
tunaliifadhi), amefikishwa mbele ya Hakimu Mkazi Devota Kisoka kwa kosa
kudhalilisha na kukojolea kitabu kitakatifu cha dini ya Kiislamu
,Oktoba 10 mwaka huu, huko Mbagala.
Oktoba:16:Walichoma makanisa Mbagala watinga kortini
Mkurugenzi
wa Mashtaka (DPP), amefungua kesi nne kwa mpigo katika Mahakama ya
Hakimu Mkazi Kisutu kwa washtakiwa tofauti ambao wanakabiliwa na makosa
ya kuchoma moto makanisa Mbagala, wizi,uharibu wa mali za watu na
unyang’nyi wa kutumia silaha katika vurugu za kidini zilizotokea Oktoba
10 mwaka huu huko Mbagala.
Septemba 10: Kesi ya Kibanda yashika kasi
Hatimaye
upande wa Jamhuri katika kesi ya kuandika na kuchapisha makala ya
uchochezi inayomkabili Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Tanzania Daima,
Absalom Kibanda na wenzake katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es
Salaam, uliupatia upande wa utetezi nakala ya mlalamikaji katika kesi
hiyo kama ulivyokuwa umeamriwa na mahakama hiyo kufanya hivyo.
Septemba 10: Mpendazoe amgwaya Dk.Mahanga
Jaji
Mkuu wa Tanzania, Mohamed Chande Othman ameliondoa Mahakama ya Rufani
nchini,ombi la kusudio la kukata rufaa iliyowasilishwa Mahakama hapo, na
Kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Fredy Mpendazoe
lilokuwa likitaka kupinga hukumu ya Mahakama Kuu ambayo ilitamka kuwa
Mbunge wa jimbo la Segerea(CCM), Dk.Makongoro Mahanga kuwa ni mbunge
halali, kufuatia wakili wa Mpendazeoe, Peter Kibatala kuwasilisha ombi
la kuiomba mahakama hiyo iondoe kusudio hilo lilokuwa limewasilishwa na
mteja wake.
Septemba 6: Dowans yaibwaga tena Tanesco
Mahakama
Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imetupilia ombi la Shirika la Umeme
(TANESCO) lilolokuwa likiomba mahakama hiyo iwapatie ruhusa ya kwenda
kukata rufaa mahakama ya rufaa ya kupinga itoe amri ya kuzuia utekelezwa
wa ukazaji wa hukumu ya mahakama hiyo ambayo iliruhusu tuzo ya Dola za
Kimarekani 65,812,630.03 iliyotolewa na Mahakama ya Kimataifa ya
Usuluhishi wa migogoro ya Kibiashara (ICC) Novemba 15 mwaka 2010 kwa
kampuni ya Dowans Hodlings SA(Costa Rica)Dowans Tanzania LTD isajiliwe
hapa nchini.
Septemba 5: Serukamba aibwaga Chadema
Mahakama ya rufaani nchini, imetupilia mbali kwa gharama maombi ya kufanyiwa mapitio ya hukumu iliyotolewa na Mahakama Kuu Kanda ya Tabora Machi 28 mwaka huu, ambayo ilisema kuwa taratibu za sheria ya uchaguzi na matokeo ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 yaliomtangaza Peter Serukamba (CCM), kuwa Mbunge wa Kigoma Mjini, hayakukiuka sheria.
Agosti 21:Mahakama yatengua ubunge wa Dk.Kafumu
Mahakama Kuu Kanda ya Tabora imemvua ubunge aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Igunga(CCM), Dk.Dalali Kafumu kwa maelezo kuwa taratibu za sheria za uchaguzi zilikiukwa katika kampeni za uchaguzi wa jimbo hilo.
Septemba: Polisi alimua Daudi Mwangosi kortini
Askari polisi Pasificus Cleophace Simon (23) amefikishwa katika
Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoani Iringa kwa tuhuma ya kumuua mwandishi
huyo katika hafla ya ufunguzi wa matawi ya Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (CHADEMA) katika Kijiji cha Nyololo, Wilaya ya Mufindi, mkoani
Iringa, uliofanyika Septemba 2, mwaka huu.
Agosti 22:Mramba nilisamehe kodi kwa amri ya Rais Mkapa
Basil
Mramba (71), Waziri mwandamizi aliyetumikia awamu nne zote za nchi hii
katika wizara mbalimbali, jana alianza kujitetea dhidi ya kesi ya
matumizi mabaya ya ofisi na kumtaja Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa, kuwa
ndiye aliyemuagiza kutoa msamaha wa kodi kwa Kampuni ya Alex Stewart.
Agosti 10: Papa Msoffe kortini kwa mauji
Mfanyabaishara maarufu jijini Dar es Salaam, mfanyabaishara maarufu jijini Marijani Abdubakari Msoffe(50) maarufu kwa jina la “Papa Msoffe chuma cha reli akishi kutu’ amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa kosa la kumuua kwa kukusudia Onesphory Kitoli.Hadi sasa Msoffe ambaye ameamishiwa gereza la Ukonga anaendelea kusota rumande kwasababu kesi inayomkabili haina dhamana.
Agosti 9:Mahalu, Mkapa wambwaga Kikwete
Mahakama
ya Hakimu Mkazi Kisutu , imemwachilia huru aliyekuwa Balozi wa Tanzania
nchini Italia, Profesa Costa Mahalu na aliyekuwa Meneja Utawala na
fedha Grace Martin waliokuwa wakikabiliwa na kesi ya wizi wa Euro
milioni mbili kutokana na ushahidi wa jamhuri kushindwa kuwatia hatiani.
Hukumu
hiyo inaweza kutafsiriwa kama ni kubwagwa kwa serikali ya Rais Jakaya
Kikwete, kutokana na hatua ya Rais mstaafu Benjamin Mkapa kukubali
kupanda kizimbani na kumtetea Mahalu dhidi ya serikali, tukio ambalo ni
la kwanza katika historia ya nchi hii. Hukumu hiyo ya kihistoria ya kesi
ya uhujumu uchumi Na.1/2007 ilitolewa jana Hakimu Mfawidhi wa mahakama
hiyo Ilvin Mugeta.
Agosti 2: Mahakama yasema mgomo wa walimu ni batili
Mahakama
Kuu Divisheni ya Kazi jijini Dar es Salaam, imesema mgomo wa walimu ni
batili kwasababu haukuzingatia matakwa ya kifungu cha 84(1),(2) cha
Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazi ya mwaka 2004 na uliandaliwa kwa
dhamila mbaya. Jaji Sophia Wambura ndiye aliyetoa uamuzi huo ambapo katika uamuzi wake huo pia aliwataka walimu wote kurejea mara moja kazini.
Julai 18:Kakobe akwaa kisiki mahakamani
Mahakama
Kuu Kanda ya Dar es Salaam imetupilia mbali pingamizi lililowekwa na
Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBC) Zakaria
Kakobe dhidi ya wachungaji wa tatu wa kanisa hilo waliomfungulia kesi ya
ubadhirifu wa fedha za kanisa hilo. Kesi hiyo namba 79/2011
ilifunguliwa Mei 26 mwaka 2011 na wachungaji watatu wa kanisa hilo,
Mchungaji Deuzidelius Patrick, Angelo Mutasingwa na Benedict Kaduma.
Wachungaji hao wanamtuhumu Askofu Kakobe kuwa amekuwa akifanya
ubadhirifu wa fedha wa kanisa hilo Sh.bilioni 14 14 na anakiuka matakwa
ya Katiba ya kanisa hilo.
Julai 24: Maranda,Farijala wafungwa tena
Mahakama
ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, kwa mara ya pili tena imemuhukumu
Kada wa Chama cha Mapinduzi(CCM), Rajabu Maranda na mpwa wake Farijala
Hussein imewahukumu kwenda jela miaka mitatu kila mmoja kwasababu
imewakuta na hatia ya makosa sita likiwemo kosa la kujipatia Shilingi
bilioni mbili kwa njia ya udanganyifu toka katika Akaunti ya Madeni ya
Nje(EPA) ya Benki Kuu ya Tanzania kwa njia ya udanganyifu.
Sambamba
na kutiwa hatiani na mahakama hiyo pia Mwenyekiti wa jopo la Mahakimu
Wakazi waliokuwa wakisikiliza kesi Jaji Fatma Masengi alitoa hukumu yake
peke yake inayotofautiana na wanajopo wenzie ambao ni Hakimu Mkazi
Projest Kayohza na Catherine Revocate ambayo iliwaachiria huru
washitakiwa na ambapo hukumu ya Jaji Masengi imebaki kuwa katika
kumbukumbu za mahakama na hukumu ya mahakama ni ile iliyotolewa na
mahakimu hao wawili kwasababu sheria inasema wengi wape.
Julai 13:Aliyemjeruhi Dk.Ulimboka kortini
MTU
mmoja ambaye ni raia wa Kenya,Joshua Mulundi(21) alifikishwa katika
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu , akikabiliwa na makosa ya kumteka na
kutaka kumuua Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari, Dk.Steven Ulimboka. Wakili
wa serikali Ladslaus Komanya mbele ya Hakimu Agnes Mchome, alidai kuwa
Mulundi ambaye makazi yake Murang'a nchini Kenya anadaiwa kuwa Juni 26
mwaka huu, akiwa eneo la Leaders Club alimteka Dk. Ulimboka. Komanya
alidai shitaka la pili ni kuwa Juni 26 mwaka huu, akiwa katika eneo la
Msitu wa Mwabepande Tegeta, Dar es Salaam kinyume na sheria mshitakiwa
huyo alijaribu kumsababishia kifo Dk. Ulimboka. Hakimu Mchome alisema
mshtakiwa hatakiwi kujibu chochote kwa sababu mahakama
hiyo haina mamlaka ya kusikiliza shauri hilo, kwani Mahakama Kuu ndiyo
yenye mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo.
Julai 11:Ndoa ya Dk.Slaa yapingwa mahakamani
Mke
wa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema), Rose
Kamili Slaa nee Sukum amefungua kesi ya madai kati ya Mahakama Kuu Kanda
ya Dar es Salaam, akiomba mahakama hiyo imzuie mumewe Dk.Willibrod Slaa
asifunge ndoa na mchumba wake Josephine Mushumbusi.
Julai 11:Mahalu hana hatia-Mawakili
Aliyekuwa Balozi
wa Tanzania nchini Italia Profesa Costa Mahalu na Meneja Utawala na
Fedha, Grace Martin wameiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es
Salaam, isiwaone wanahatia katika kesi ya wizi wa Euro Milioni tatu
kwasababu upande wa Jamhuri umeshindwa kuleta ushahidi wa kutenda makosa
hayo.
Julai 12:Mahalu ana hatia-Serikali
Upande
wa Jamhuri katika kesi wizi wa Euro milioni mbili inayomkabili
aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia, Profesa Costa Mahalu na
Grace Martin wamiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam,
iwaone washitakiwa hao wana hatia kwa sababu washitakiwa wameshindwa
kuleta ushahidi mathubuti ambao unaonyesha hawakutenda makosa hayo.
Julai 10:Rais wa Madaktari afikishwa mahakamani
Rais
wa Chama cha Madaktari nchini(MALT), Dk.Namala Mkopi jana alifikishwa
katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam,chini ya ulinzi
mkali wa polisi akikabiliwa na makosa mawili likiwemo kosa la kudharau
amri halali ya Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi.
Julai 2:Vigogo Suma JKT kortini
Mkurugenzi
wa Shirika Jeshi la Kujenga Taifa (SUMA JKT) Kanali Ayoub Mwakang’ata
na maofisa wenzake sita wa jeshi hilo jana walifikishwa katika Mahakama
ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam wakikabiliwa na mashitaka saba ya
kula njama na matumizi mabaya ya madaraka. Mbali na Kanali
Mwakang’ta washitakiwa wengine ni Luteni kanali Mkohi Kichogo,Luteni
Kanali Paul Mayavi,Meja Peter Lushika,Sajenti John Lazier,Meja Yohana
Nyichi na Mkurugenzi wa Miradi ya Matrekta wa SUMA JKT-Luteni Kanali
Felex Samillan. Mawakili toka ofisi ya Kuzuia na Kupamba na
Rushwa(TAKUKURU), Dominsian Kessy na Ben Lincoln walidai mbele ya Hakimu
Mkazi Alocye Katemana na kuwa kosa la kwanza ni la matumizi mabaya ya
madaraka kinyume na
kifungu cha 31 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ya mwaka
2007, inayowakabili washitakiwa wote. Wakili Kessy alidai kuwa Machi 5
mwaka 2009 katika chumba cha mikutano cha ofisi ya SUMA JKT Dar es
salaam,wakiwa ni wajumbe wa bodi na Bodi ya Tenda ya SUMA JKT kwa
makusudi walitumia madaraka yao vibaya kwa kutoa maamuzi ya bodi hiyo
ambayo yaliyoonyesha yametolewa na TAKOPA kwa madhumuni ya kununua
magari na vifaa vya ujenzi bila kupata idhini ya kutoka Bodi ya ya
Wakurugenzi ya TAKOPA.
Julai 23:Tindu Lissu ashinda kesi ya kupinga ubunge wake
Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma imetupilia mbali
kesi ya kupinga ubunge wa Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki
CHADEMA,Tundu Lissu kwa maelezo kuwa mbunge huyo kesi hiyo haina mantiki
yoyote.
Julai 17; Vigogo wa Deci wana kesi ya kujibu
WAKURUGENZI
watano wa Taasisi ya Kusimamia na Kuendesha Upatu (Deci), wanaokabiliwa
na kesi ya kuendesha shughuli za upatu bila kibali wamepatikana na kesi
ya kujibu dhidi ya mashtaka yanayowakabili katika Mahakama ya Hakimu
Mkazi Kisutu.
Julai 28:Vigogo Bodi ya PSPT kortini
Mkurugenzi
Mtendaji wa Bodi ya Watalaam wa Manunuzi na Ugavi (PSPT), Clemence
Tesha na wenzake jana walijikuta wakifikishwa katika Mahakama ya Hakimu
Mkazi Kisutu Dar es Salaam, wakikabiliwa na makosa ya matumizi mabaya ya
madaraka.
Juni 4:Mbunge Badwel kortini kwa rushwa
Mbunge wa
Jimbo la Bahi(CCM), Omary Ahmed Badwel(43) jana alijikuta akifikishwa
katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam,na Taasisi ya
Kuzuia na Kupambana na Rushwa(Takukuru), kwa makosa ya rushwa ya
shilingi Milioni moja toka kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya
Mkuranga,Jonathan Liana.Kesi hivi sasa imefikia hatua ya mashahidi wa
upande wa jamhuri kuendelea kutoa ushahidi wao.
Juni 27:Mramba,Yona na Mgonja wana kesi ya kujibu
Mahakama
ya Hakimu Mkazi Kisutu imewaona mawaziri wa zamani Basil Mramba,Daniel
Yona na Katibu Mkuu Mstaafu wa Wizara ya Fedha, Gray Mgonja kuwa wana
kesi ya kujibu.
Mei 8:Garce Martin atoa utetezi
Mshtakiwa
wa pili katika kesi ya uhujumu,Grace Martin ameiomba mahakama ya Kisutu
imuone hana hatia kwa mashtaka yote yanayomkabili kwasababu hakutenda
makosa hayo wakati akiwa na wadhifa wa Meneja Utawala na Fedha wa
Ubalozi wa Tanzania nchini Italia.
Mei 7:Rais Mkapa amkaanga JK mahakamani
RAIS
mstaafu, Benjamin Mkapa, jana aliikaanga serikali ya Jakaya Kikwete
mahakamani akidai kuwa hakuna ubadhirifu wowote uliofanywa na aliyekuwa
Balozi wa Italia, Prof. Costa Mahalu, katika ununuzi wa jengo la ubalozi
nchini humo.
Akiongozwa
na wakili wa utetezi, Alex Mgongolwa, baada ya kuapa alieleza kuwa kati
ya mwaka 1995-2005 akiwa Rais alifahamu ununuzi wa jengo la ubalozi
nchini Italia kwa euro 3,098,741.40, na kuwa hata aliyekuwa Waziri wa
mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ambaye ni Rais wa sasa, Jakaya
Kikwete alikubaliana na ununuzi huo.
Mkapa
ambaye ni shahidi wa Mahalu katika kesi hiyo alisema mwaka 2003 yeye
ndiye aliyekwenda mjini Rome-Italia kulizindua jengo hilo la kisasa,
Profesa Mahalu akiwa balozi.
“Serikali
yangu iliarifiwa bei na taratibu za kulinunua na mimi kama Rais wa nchi
nilitaarifiwa kuwa muuzaji alitaka malipo yafanywe mara mbili tofauti
katika akanti zake …na mimi kwa niaba ya serikali yangu nikatoa idhini
linunuliwe kwa mtindo huo nilioutaja hapo juu,” alidai Rais Mkapa.
Mei 2: Dk.Mahanga ashinda kesi
Mahakama
Kuu Kanda ya Dar es Salaam imetupilia mbali kesi ya kupinga ubunge wa
Mbunge wa Jimbo la Segerea(CCM), Dk.Makongoro Mahakanga iliyokuwa
imefunguliwa na alikuwa mgombea kiti hicho kwa tiketi ya (Chadema), Fred
Mpendazoe kwa maelezo kuwa kesi hiyo haina mantiki kisheria na mahakama
hiyo kumtangaza Dk.Mahanga kuwa ndiye mbunge halali wa jimbo hilo.
Mei 29:Mamia wamzika wakili Stanslaus Boniface
Mkurugenzi wa
Mashitaka nchini,Dk.Eliezer Feleshi amemwelezea aliyekuwa Mkurugenzi
Msaidizi wa mashitaka marehemu Stanslaus Boniface(44) ,kuwa alikuwa ni
mtumishi aliyejituma ,mwadilifu na aliyekuwa na ushirikiano na watumishi
wa kada zote bila kujali umri wala cheo chake. Dk.Feleshi
aliyasema hayo leo katika ibada ya kuuga mwili wa marehemu Boniface
iliyofanyika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, na kisha mwili wa marehemu
ulizikwa katika makaburi ya Kinondoni.
Mei 29:Idd Simba aburuzwa kortini
Hatimaye sakata
la ufisadi katika Shirika la Usafirishaji Dar es Salaam(UDA), lilifikia
tamati kwa serikali kumfikisha Mahakama ya Hakimu Mkazi
Kisutu,Mwenyekiti wa Bodi ya shirika hilo Idd Simba kwa makosa ya
kughushi,kujipatia fedha kwa njia ya udangayanyifu na kulisababishia
shirika la Usafiri Dar es Salaam(UDA) Ltd shilingi bilioni 2.3. Mbali
na Simba ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya UDA ,wengine ni Mkurugenzi
Salim Mwaking’inda na Meneja Mkuu wa shirika hilo Victor Milanzi.
Mei 27:Wakili maarufu Stanslaus Boniface ‘Jembe’afariki
Mkurugenzi Msaidizi
wa ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka nchini, Stanslaus Boniface Makulilo
(44) ‘Jembe’ amefariki ghafla usiku wa kuamkia jana katika Hospitali ya
Regency jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi
wa Mashitaka nchini(DPP), Dk.Eliezer Feleshi alilithibishia Tanzania
Daima jana asubuhi kutokea kwa kifo hicho ambapo alisema bado ofisi yake
na taifa limepata pigo kubwa lakuondokewa na gwiji hilo la uendeshaji
wa mashitaka hususani ya jinai hapa nchini na kwamba mchango wake mzuri
katika uendeshaji wa kesi hususani za jinai hautasaulika na utaenziwa.
Dk.Feleshi
alikuwa akizungumza na gazeti hili kwa uzuni alisema Jumamosi jioni
Boniface ambaye pia alikuwa Msimamizi wa Uendeshaji wa Kesi zenye
maslahi kwa umma, aliingia Dar es Salaam, akitokea Moshi kwaajili ya
kutoa mafunzo ya jinsi ya uendeshaji wa mashitaka kwa maofisa wa Idara
ya Uhamiaji akiwa mwenye afya njema na alirejea nyumbani kwake Kinondoni
lakini ilipofika usiku wa siku hiyo hali yake ilibadilika ghafla na
kukimbizwa katika Hospitali ya Regency kwaajili ya matibabu.
Mei 31:Kajala alia asema Segerea siyo sehemu ya matanuzi
Msanii wa
filamu nchini, Kajala Masanja, jana alimwaga machozi na kuujia juu
upande wa jamhuri katika kesi inayomkabili ya utakatishaji fedha haramu
katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, akiushinikiza
ulete mashahidi haraka kwani mahabusu anakoishi siyo sehemu ya starehe. Kajala
alitoa shinikizo hilo mbele ya Hakimu Mkazi, Sundi Fimbo, muda mfupi
baada ya wakili wa Taasisi ya Kuzuia na Kupamba na Rsuhwa (TAKUKURU),
Leonard Swai, kuikumbukusha mahakama kuwa kesi hiyo ilikuja jana kwa
ajili ya upande wa jamhuri kuanza kutoa ushahidi wao, lakini akadai hilo
halitaweza kufanyika, kwa sababu hajaja na
mashahidi na anaomba kesi hiyo iahirishwe. Baada ya wakili huyo
kumaliza kutoa maelezo hayo, ndipo Kajala akanyosha kidole na kuomba
ruhusa ya mahakama ili aweze kuzungumza jambo. “Mheshimiwa hakimu, hivi
huyu wakili wa serikali anafikiri kule Segerea ninakoishi kwa sasa ni
sehemu ya starehe? Mahabusu kunatisha, wewe wakili wa serikali lete
mashahidi kesi isikilizwe,” alidai Kajala huku akitokwa na machozi.
Mei 24:Mnyika ambwaga Ng’umbi kortini
Hatimaye Mahakama
Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imepigilia msumari wa mwisho kwa kusema
kuwa Mbunge wa Jimbo la Ubungo kwa tiketi ya (Chadema), John Mnyika
ndiye mbunge halali wa jimbo hilo na matokeo ya uchaguzi ya jimbo hilo
yaliyotangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi Novemba mwaka 2010,yalikidhi
matakwa ya kisheria.
Aprili 30:Mahakama yatengua ubunge wa Aeshi Hillal
Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga imetengua ubunge wa aliyekuwa mbungu wa
Jimbo la Sumbawanga Mjini(CCM), Aeshi Hillali ililiyokuwa imefunguliwa
na aliyekuwa mgombea wa Chadema, katika uchaguzi mkuu uliopita ambaye
alikuwa akiomba mahakama hiyo mvue ubunge kwasababu alishindwa kwa hira.
Aprili 23: Waziri Ntagazwa kortini kwa udanganyifu
Aliyekuwa Waziri
mwandamizi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa awamu
tofauti Arcado Ntagazwa(65) amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi
Kisutu Dar es Salaam, kwa kosa moja tu la kujipatia kofia,fulana zenye
jumla ya thamani ya shilingi milioni 74.9 kwa njia ya udanganyifu.
Aprili 5:Lema avuliwa ubunge na mahakama
Mahakama
Kuu Kanda ya Arusha imetoa hukumu ya kumvua ubunge aliyekuwa Mbunge wa
Arusha Mjini(Chadema), baada ya kumtia hatiani kwa makosa ya kutoa lugha
ya udhalilisha katika kampeni za uchaguzi mkuu wa jimbo hilo mwaka
2010.
Machi 27: Hakimu Waliarwande Lema akataliwa na Jamhuri
Mawakili wa
Serikali katika kesi ya jinai Na.149/2010 ya utakatishaji fedha haramu
ya zaidi ya Shilingi bilioni 3.8 inayomkabili Afisa wa Mamlaka ya
Mapato(TRA), Justice Katiti na wenzake,katika Mahakama ya Hakimu Mkazi
Kisutu Dar es Salaam, jana waliwasilisha ombi la kumuomba Hakimu Mkazi
anayesikiliza kesi hiyo Waliarwande Lema ajitoe kwenye kesi hiyo
kwasababu hawana imani naye.
Machi 27:Mawakili Mramba hana kesi ya kujibu
Aliyekuwa
Waziri wa Fedha, Basil Mramba ameiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu
Dar es Salaam, imuone hana kesi ya kujibu na afutiwe kesi inayomkabili
ya matumuzi mabaya ya ofisi ya umma na kuisababishia serikali hasara ya
Shilingi bilioni 11.7 kwasababu upande wa Jamhuri katika kesi hiyo
umeshindwa kuthibitisha kesi yake bila kuacha mashaka.
Machi 22:Mtikila amkataa hakimu Fimbo
Ikiwa ni
siku chache baada ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu,
Sundi Findo, atoe uamuzi wa kumuona Mwenyekiti wa chama cha
Democratic(DP), Mchungaji Christopher Mtikila ana kesi ya kujibu katika
kesi ya kuchapisha na kusamba waraka wa uchochezi dhidi ya Rais Jakaya
Kikwete , Mtikila amewasilisha mahakamani hapo ombi la kumuomba hakimu
huyo ajitoe kwenye kesi yake ya jinai Na.132/2011 kwasababu hawezi
kumtendea haki.
Machi 15: Kajala kortini kwa utakatishaji fedha
Msanii wa filamu nchini, Kajala Masanja na mumewe, walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na makosa ya utakatishaji fedha haramu.
Machi 15:Mashahidi 10 kumvaa Liyumba
Upande
wa Jamhuri katika kesi ya kukutwa na simu gerezani inayomkabili
aliyekuwa Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala wa Benki Kuu ya Tanzania,
Amatus Liyumba umeiambia Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam,
kuwa unatarajia kuleta jumla ya mashahidi 10 na vielelezo 10 katika kesi
hiyo siku itakapoanza kusikilizwa.
Machi 13:Mtikila anaswa kesi ya kumwita JK gaidi
Hatimaye Mahakama
ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, imesema Mwenyekiti wa Chama cha
Democratic Part(DP), Mchungaji Christopher Mtikila ana kesi ya kujibu
katika kesi ya kuchapisha na kuusambaza waraka wa uchochezi dhidi ya
Rais Jakaya Kikwete.
Machi 7:Kibanda abadilishiwa hati ya mashtaka
Upande wa Jamhuri katika kuchapisha makala ya uchochezi inayomkabili Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Tanzania Daima,
Absalom Kibanda na mwandishi Samson Mwigamba jana ulishindwa kuwasomea
maelezo ya awali washtakiwa hao na badala yake umeibadilisha hati ya
mashtaka na pia kumuongeza mshtakiwa mmoja ambaye ni Mhariri Mtendaji wa
Kampuni ya Mwananchi Comunication, Theophil Makunga.
Machi 31:JK alinipa idhini ya kununua jengo la ubalozi-Mahalu
Aliyekuwa Balozi
wa Tanzania nchini Italia, Profesa Costa Mahalu ameieleza Mahakama ya
Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, Rais Jakaya Kikwete ndiye aliyempatia
mamlaka ya kisheria (Special Power of Attoney) ya kununua jengo la
Ubalozi wa Tanzania nchi Italia kwa kutimia njia ya mikataba miwili kwa
thamani ya Euro 3,098,034.Mahalu alitoa madai hayo wakati akimaliza
kutoa ushahidi wake leo.
Februali 23: Washtakiwa kesi ya ‘Samaki wa Magufuli’jela miaka 30
Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imeandika historia
mpya kwa hatua yake ya kuwatia hatiani washtakiwa wawili wa kesi ya
uvuvi haramu katika Ukanda wa Tanzania maarufu ‘Kesi ya Samaki wa
Magufuli’ na kuwahukumu kwenda jela jumla ya miaka 30 au kulipa faini ya
jumla ya Shilingi bilioni 22.
Sambamba na hilo mahakama hiyo imeridhia ombi Kiongozi wa jopo la mawakili wa serikali lilokuwa likiongozwa na Wakili Mkuu wa Serikali Biswalo Mganga aliyekuwa akisaidiwa na Dk.Deo Nangela ,Prosper Mwangamila na Hamidu Mwanga aliloliwasilisha chini ya kifungu cha 351 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya mwaka 2002 , ambalo aliomba mahakama hiyo itoe amri ya meli hiyo kutaifishwa na serikali ya Tanzania.
Sambamba na hilo mahakama hiyo imeridhia ombi Kiongozi wa jopo la mawakili wa serikali lilokuwa likiongozwa na Wakili Mkuu wa Serikali Biswalo Mganga aliyekuwa akisaidiwa na Dk.Deo Nangela ,Prosper Mwangamila na Hamidu Mwanga aliloliwasilisha chini ya kifungu cha 351 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya mwaka 2002 , ambalo aliomba mahakama hiyo itoe amri ya meli hiyo kutaifishwa na serikali ya Tanzania.
Februali 20:Dowans yaibwaga tena Tanesco
Mahakama
Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imetupilia mbali ombi la Shirika la Umeme
(TANESCO) lilokuwa linaomba mahakama iwaruhusu kukata rufaa katika
Mahakama ya Rufaa nchini kupinga hukumu ya Mahakama Kuu iliyotolewa
Septemba 28 mwaka jana,ambayo iliruhusu tuzo ya Kampuni ya Dowans
iliyopewa na Mahakama ya Kimataifa ya Usuhuhishi wa migogoro ya
Kibiashara(ICC) isajiliwe hapa nchini kwasababu hiyo haina mamlaka ya
kuwaruhsu kwenda katika mahakama hiyo ya juu nchini.
Januari 23: Jela kwa kuiba Power Windor mahakamani
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ,imemhukumu kifungo cha miaka mitano jela, Deogratius Owiso baada ya kumkuta na hatia ya kuiba Power windor katika gari lenye usajili Na.T 331 BHY aina ya Toyota Land Cruser mali ya Adrian Muyungi, lilokuwa limeegeshwa katika eneo hilo la mahakama hiyo.
Januari 13: Mgombea urais wa upinzani Burundi afikishwa mahakamani Kisutu
Aliyekuwa mgombea
urais wa chama kimoja cha upinzani nchini Burundi, Alex Sinduhnje, jana
alifikishwa katika mahabusu ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es
Salaam, lakini hata hivyo hakuweza kupandishwa kizimbani.
Januari 11:Wanafunzi UDSM waenda jela kwa kukosa dhamana
Wafunzi wanne
kati ya 51 wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), wanaokabiliwa na
kesi ya kufanya mkusanyiko haramu wamepelekwa rumande baada ya kushindwa
kukamilisha masharti ya dhamana waliyopewa.
Waliopelekwa rumande ni Elias Mwambapa, Alphonce Lusako, Moris Denis na Jabir Ndimbo ambao walishindwa kukamilisha masharti ya dhamana ya kuwa na mdhamini mmoja wa kuaminika na kusaini hati ya dhamana ya Sh 1 milioni kwa kila mshtakiwa.
Waliopelekwa rumande ni Elias Mwambapa, Alphonce Lusako, Moris Denis na Jabir Ndimbo ambao walishindwa kukamilisha masharti ya dhamana ya kuwa na mdhamini mmoja wa kuaminika na kusaini hati ya dhamana ya Sh 1 milioni kwa kila mshtakiwa.
Januari 10:Hamad Rashid atia kitanzi CUF kortini
Hatimaye mbunge
wa Wawi Hamad Rashid Mohamed(CUF), na wenzake 10 jana waliwasilisha
maombi madogo katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, wakiomba
mahakama hiyo itamke kuwa uamuzi wa Baraza la Uongozi Taifa la chama
hicho uliomvua uanachama yeye na wenzake ni batili.
Januari 10: Raia wa Burundi kortini kwa kukutwa na risasi 682
Raia wa
Burundi, Ismail Stefano (39) jana alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu
Mkazi Kisutu Dar es Salaam, akikabiliwa na mashtaka ya kukutwa na
silaha mbili aina ya SMG na risasi 682.
Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika;
0 comments:
Post a Comment