NUSU ya watu wanaotumia kondomu kwa ajili ya kujikinga na mimba
ama magonjwa ya zinaa, hawajui namna ya kuitumia mipira hiyo, utafiti
umeeleza.
Utafiti
huo mpya ulifanywa na Dk Stephanie Sanders wa Taasisi ya Kinsley
inayohusika na Utafiti wa Masuala ya Jinsia, Jinsi na Uzalishaji katika
Chuo Kikuu cha Indiana.
Kwa
mujibu wa utafiti huo uliofanywa katika nchi 14 ikiwamo Tanzania katika
kipindi cha miaka 16 iliyopita kuanzia mwaka 1995 hadi 2011, watu wengi
wamekuwa wakifanya makosa kwa namna mbalimbali katika kutumia kandomu
ikiwamo uvaaji.
“Makosa
yanayofanywa mara kwa mara na watumiaji wa kondomu ni pamoja na
kuingiza kinga hiyo nusu katika uume wakati wa ngono au kuitoa kabla
tendo hilo halijamalizika au kusubiri mpaka isinyae,” imesema sehemu ya
utafiti huo.
Makosa mengine ni kutoacha nafasi katika ncha ya kondomu kwa ajili ya mbegu za kiume na kuzifungua vibaya katika pakiti yake.
Jambo hilo linalosababisha kucha kuzitoboa na hatimaye kupitisha mbegu au majimaji kwenda kwa mwanamke,” umeeleza utafiti huo.
Utafiti
huo umeonyesha kuwa makosa mengine ni kuigeuza kondomu ndani-nje,
kuihifadhi katika sehemu isiyostahili na kurudia kuitumia katika tendo
lingine la ngono.
Kuivua
vibaya: Asilimia 57 ya watu waliohojiwa, walikiri kuvua kondomu
kimakosa baada ya tendo la ngono. Kati yao asilimia 27 walikuwa
wanawake na asilimia 31 ni wanaume.
Pamoja
na makosa hayo ya uvaaji wa kondomu, watafiti nchini India wanatarajiwa
kufanya utafiti mwingine mkubwa kuhusu suala hilo kubaini sababu yake.
Watafiti
hao waliamua kufanya uchunguzi baada ya kubainika kuwapo kwa wanaume
ambao maumbile yao ni makubwa au madogo kuliko mipira hiyo ya kiume.
Hata hivyo, kondomu zinazopatikana nchini Tanzania hazitofautiani ukubwa.
Dk
Sanders alisema makosa yanayofanywa wakati wa kutumia mipira hiyo
yanachochewa na watumiaji wenyewe na kukosekana kwa msisitizo wa elimu
ya namna ya kuzitumia kondomu hizo kutoka kwa watengenezaji au taasisi
za Ukimwi.
Makundi tofauti yalijumuishwa katika utafiti huo wakiwemo wanandoa, wafanyabiashara ya ngono na wanafunzi wa vyuo.
Kati
ya asilimia 17 na 51.1 ya watu walioulizwa maswali katika utafiti huo
walikiri kuwa huingiza kondomu nusu katika uume wakati wa tendo la
ngono.
chanzo :mwananchi
0 comments:
Post a Comment