Lulu akisindikizwa na askari Magereza.
Lulu akiingia katika gari la Magereza kwenda Rumande
Gari lililomleta Lulu likiondoka mahakamani leo.Picha Zote na Habari na Mdau Dande Francis
---
DAR ES SALAAM, Tanzania
HATIMAYE
Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, leo ilimpatia masharti matano ya
kupata dhamana kwa msanii wa Filamu nchini Elizabeth Michael ‘Lulu’, anayekabiliwa na kesi ya kuua bila kukusudia aliyekuwa msanii mwenzake marehemu Steven Kanumba.
Masharti
hayo yaliyolewa jana na Jaji Zainabu Mruke muda mfupi baada ya mawakili
wa Lulu, Peter Kibatara, Kennedy Fungamtama na Fulgence Massawe kuiomba
mahakama hiyo impatie dhamana mshtakiwa huyo ambaye anasota rumande
tangu April mwaka jana ambapo walieleza kuwa ombi la dhamana wameliwasilisha chini ya kifungu cha
148(1) ,(2) Cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya mwaka 2002 .
Jaji
Mruke alisema ili mahakama impatie dhamana ni lazima asalimishe kwa
Msajili wa mahakama hiyo hati ya kusafiria, kutotoka nje ya Dar es
Salaam bila ruhusa ya mahakama, kuripoti kwa msajili kila mwezi ,kuwa
na wadhamini wawili ambao ni watumishi wa serikali ambao watasaini
bondi ya Sh.milioni 20 kila mmoja.
Baada
ya jaji huyo kutangaza masharti hayo Lulu na wakili wake walitoka nje
ya ukumbi uliokuwa ukiendeshwa kwa shauri hilo kwa ajili ya kwenda kwa
msajili kutimiza masharti hayo lakini kwa bahati mbaya Msajili hakuwepo
ofisini na hivyo kufanya Lulu kurudishwa rumande hadi leo atakapoletwa
kwa ajili ya kujatimiza masharti hayo mbele ya Msajili wa mahakama hiyo.
Kufuatia
mahakama hiyo jana kumpatia masharti ya dhamana Lulu kutoka na ombi
lake Na.125/2012 la kuomba mahakama hiyo impatie dhamana, lakini bado
kesi ya msingi inayomkabili Lulu ambayo ni ya kuua bila kukusudia bado
haijapangiwa jaji wala tarehe ya kuanza kusikilizwa.
Desemba
21 mwaka jana , Hakimu Mkazi Christine Mbando wa Mahakama ya Hakimu
Mkazi Kisutu aliifunga kesi ya kuua bila kukusudia Lulu na kuiamishia
rasmi kesi hiyo katika Mahakama Kuu, na uamuzi huo wa mahakama ulitokana
na upande wa Jamhuri kumsomea maelezo ya kesi yake kwa kina mshtakiwa
huyo na kuieleza mahakama kuwa wanakusudia kuleta jumla ya mashahidi
tisa.
0 comments:
Post a Comment