Mtuhumiwa wa nyara za serekali Peter
Laurence mwenye kofia katikati akiwa na maofisa wa jeshi la polisi
chini ya ulinzi ,eneo la kisongo mtaa wa mateves nje kidogo ya jiji la
Arusha baada ya kukamatwa na shehena ya nyara za serikali nyumbani
kwake
Miongoni mwa nyara za serikali zilizokuwa zimehifadhiwa kwenye ghala maalumu kwenye nyumba ya mtuhumiwa Peter
Lawrence zikionekana kwenye maboksi tayari kwa kusafirishwa nje ya
nchi.
--
Na Bertha Ismail-Arusha
JESHI la polisi mkoani
Arusha,limekamata shehena kubwa ya nyara mbalimbali za serikali
zilizokuwa zimehifadhiwa kwenye ghala maalumu,eneo la Matevesi Kisongo
nje kidogo ya jiji la Arusha,zikiwa tayari kwa kusafirishwa nje ya nchi.
Nyara hizo ni pamoja na Ngozi za
Simba,Chui na Mamba,meno 2 ya Tembo,vichwa vya Nyani,Swala na Nyati,Pembe
za kifaru,na zingine nyingi ambazo jeshi la polisi linaendelea
kuzitambua sambamba na thamani yake.
Pia jeshi hilo
limemtia mbaroni mtuhumiwa wa nyara hizo aliyetambulika kwa jina la
Peter Leurence(55)mkazi Ngaramtoni ya chini,ambaye alikuwa amezihifadhi nyara hizo kwenye maboksi ndani ya nyumba yake iliyopo eneo
hilo la Mateves.
Kwa mujibu wa kamanda wa polisi
mkoni Arusha,Liberatus Sabas tukio la kukamatwa kwa nyara hizo limetokea
jana(jan 6) majira ya saa 6.30 usiku wa kuamkia leo eneo la kisongo mtaa wa
mateves baada ya kupata taarifa kutoka kwa raia wema.
Kamanda Sabas alisema kuwa baada
ya jeshi hilo kupata taarifa za siri walifika
eneo la tukio na kukamata vitu hivyo.
pia Sabas alikanusha vikali taarifa za polisi kuhusika na majangili katika uwindaji lakini alikiri endapo polisi wakihusika wanachukuliwa kama wahalifu kama wahalifu wengine.
kwa upande wake ofisa kikosi cha kupambana na ujangili kanda ya kaskazini Deodatus Makene alisema thamani halisi ya vitu hivyo havijajulikana ila mabaki ya wanyama hao wanaruhusiwa kuwindwa hivyo wanachunguza tu kama uwindaji wake ni halali kwa makabrasha yake na mamlaka husika .
0 comments:
Post a Comment