Timu
ya Young Africans Sports Club imetoka sare ya bao 1-1 dhidi ya timu ya
Arminia Bielefeld ya Ujerumani katika mchezo wa kirafiki uliofanyika
leo jioni katika uwanja wa Adora Football pemebni kidogo ya mji wa
Antalya.
Armini
Bielefeld ilianza soka kwa kasi kwa lengo la kujipatia bao la mapema
lakini umakini wa walinzi wa Yanga na mlinda mlango Ally Mustafa
'Barthez' ilikuwa kikwazo kwao kwani mashambulizi yao yaliishia
mikononi mwake.
Ikiwa
ni mchezo wake wa kwanza wa kujipima nguvu Young African iliweza
kuonyesha soka safi katika kipindi cha kwanza hali iliyowashangaza
wajerumani hao na kipindi cha pili kuamua kufanya mabadiliko ya kikosi
kizima.
Viungo
wa Yanga Frank Domayo, Haruna Niyonzima na Kabange Twite waliweza
kutawala mchezo kwa dakika 45 zote za kipindi cha kwanza huku baadhi ya
wajerumani waliokuwa wakishuhudia mchezo huo kushangazwa na kiwango cha
timu ya Yanga
Hadi mapumziko timu zote zilikwenda mapumziko , Young Africans 0 - Arminia Bielefeld.
Kipindi
cha pili Arminia Bielefeld iliamua kubadilisha kikosi chake chote cha
wachezaji kwa lengo la kuingiza nguvu mpya ili waweze kuikabili kasi ya
wachezaji wa Yanga ambao walionekana kuwa imara na bora zaidi.
Dakika
ya 55 Yanga ilifanya mabadiliko kwa kuwatoa Said Bahanuzi na David
Luhende na nafasi zao kuchukuliwa na Jerson Tegete na Saimon Msuva.
Jerson
Tegete aliipatia Young Africans bao la kwanza dakika ya 60 ya mchezo,
akiunganisha pasi safi aliypewa na Saimon Msuva aliyewatoka walinzi wa
Arminia Bielefeld na kumpa pasi Tegete ambaye aliukwamisha mpira wavuni
na kuhesabu bao la kwanza.
Kuona
hivyo wajerumani walikuja juu kusaka bao la kusawazisha, lakini bado
ukuta wa Yanga uliendelea kuonekana kuwa makini lakini makosa ya mshika
kibendera yaliipelekea Armini Bielefeld kupata bao la kusawazsiha
dakika ya 81 kupitia kwa Eric Agyemang amabaye alikua ameotea.
Mpaka dakika 90 za mchezo zinamalizika Young Africans 1 - 1 Armini Bielefeld.
Kocha
Mkuu wa Young Africans Ernest Brandts amesema amefurahishwa na kiwango
walichokionyesha wachezaji wake na anaamini kadri siku zinavyokwenda
wanazidi kuimarika na kuwa bora, hivyo katika michezo mingine
wataendelea kuonyesha mabadiliko makubwa.
Young Africans:
Ally Mustafa 'Barthez, Mbuyu Twite, Oscar Joshua, Nadir Haroub
'Cannavaro', Kelvin Yondani, Kabange Twite, Haruna Niyonzima/Nizar
Khalfan, Frank Domayo/Nurdin Bakari, Said Bahanuzi/Jerson Tegete,
Didier Kavumbagu, David Luhende/Saimon Msuva
0 comments:
Post a Comment