MWANAFUNZI wa Chuo Kikuu cha Mt. Yohana,
Lyidia Mzima (57), ameuawa na watu wasiojulikana alipokuwa akitoka
kujisomea jirani na eneo la chuo.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma, David Misime, alisema jana
kuwa tukio hilo lilitokea juzi usiku na kwamba mwanafunzi huyo
alinyofolewa nyama za pajani na jeraha kichwani linaloonesha
kusababishwa na kitu chenye ncha kali.
Alisema mwili wa marehemu uligunduliwa asubuhi na wananchi ambao waliwafahamisha polisi kuhusiana na tukio hilo.
Alisema mwanafunzi huyo alikuwa amepanga nyumba katika Mtaa wa
Kibaoni-Image B, Kata ya Kikuyu Kusini, ambapo inadaiwa aliwaaga
wenzake aliokuwa akisoma nao. Kamanda huyo alisema ameanzisha msako
mkali wa kuwatafuta wauaji hao, ili kuwafikisha kwenye vyombo vya
sheria.
“Tukio hili hatutalifumbia macho, tunafanya msako mkali mara moja
na kuhakikisha wahusika wanabainika na kuchukuliwa hatua, ili liwe
fundisho kwa wengine. Natoa rai kwa watu wanaojihusisha na vitendo vya
uhalifu na mauaji kuacha mara moja kwani Jeshi la Polisi halijalala
kama wanavyofikiri,” alisema.
Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya rufaa iliyopo mkoani hapa ukisubiri kufanyiwa uchunguzi.
chanzo:Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment