Umati wa wananchi na wana CCM |
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa Jesca Msambatavangu akimkaribisha Mangula jukwaani |
Kijana aliyeshikuiliwa na polisi na kuachiwa kwa kutaka kuvuruga mkutano wa CCM leo mwenye shati jeupe |
Umati wa wananchi waliofika kumsikiliza leo |
mkuu wa mkoa wa Iringa Dr Christine Ishengoma (kushoto) akiteta jambo na Mangula leo katikati ni mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa Jesca Msambatavangu |
Mangula baada ya kuvishwa mavazi ya kichifu Iringa |
MAKAMU
mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (CCM) Tanzania Bara Philip
Mangula ametangaza kiama kwa makada wa CCM ambao wanajipitisha kwa
ajili ya kuwania udiwani,ubunge na urais mwaka 2015 kuwa wasitegemee
kupitishwa na chama hicho na kuwa kwa sasa Rais ni Jakaya Kikwete
hategemei kuona mwanachama mweingine akizunguka kuanza kampeni za
urais .
Akiwahutubia
mamia ya wakazi wa jimbo la Iringa mjini leo katika uwanja wa
Mwewmbetogwa Mangula alisema kuwa CCM kwa sasa ina ajenda moja pekee
ya kutekeleza ilani yake na sio kujibishana na vyama vya
upinzani wala makada wake kuanza kujipitisha kwa wanachama kwa
lengo la kugombea nafasi za uongozi mwaka 2015.
Mangula
alisema iwapo mwana CCM yeyote atabainika akipita kushawishi
wanachama ili kumchagua mwaka 2015 kwa nafasi yeyote ile iwe ya
udiwani ,ubunge na Urais atakuwa amepoteza muda wake kwani kamwe
hatapitishwa kuwa mgombea ila watakaopitishwa ni wale ambao
watafuata taratibu za kampeni zitakazotangazwa na chama si vinginevyo
.
"
Kuanzia sasa nawaagiza makatibu wa matawi wote nchini kuwa na
daftari la taarifa za wanachama ambao wameanza kujipitisha katika
matawi kwa ajili ya kuwania uongozi ili wakati wa kupitisha majina
ya wagombea kuweza kuwakata majina wale wote walioanza kampeni
sasa na kuwavuruga waliopo madarakani"
Alisema
kuwa chama kimekuwa kikishuhudia kuwepo kwa makundi makubwa ya
wanachama ambao wameanza kumvuruga Rais Kikwete kwa kupita huku na
kule kujionyesha kwa wanachama kwa nia ya kutaka kugombea Urais
na kuwa mgombea wa urais wa CCM hapatikani kwa vurugu kamna hivi
zinazoendelea kwa watu kujipitisha kabla ya muda.
Hivyo aliwataka wote wanaotaka kuwania uongozi
mwaka 2015 kuanzia ngazi ya udiwani ,ubunge na Uraisi kuwa na subira
hadi chama kitakapotangaza .
katika
hatua nyingine Mangula aliwataka viongozi wa vyama vya siasa
kuendelea na shughuli zao za kisiasa bila kuvuruga amani wala
kugombana na kuwa kwa sasa CCM ina agenda moja pekee ya
kuhakikisha inatekeleza ilani yake na sio
kuanza kuvutana na vyama vya upinzani.
Pia
aliwataka wana CCM jimbo la Iringa wakiwemo viongozi kuweza
kujiuliza sababu za kushindwa uchaguzi mkuu mwaka 2010 jimbo hilo
la Iringa mjini na kuwa iwapo ni pepo aliyesababisha kushindwa basi
kuhakikisha wanamkabili pepo huyo mwaka 2015.
Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi juu ya ziara ya Mangula jimbo la Iringa mjini baadhi ya wananchi walikuwa kwa
upande wake Brown Payovela alisema kuwa wakazi wa mkoa wa Iringa
wameonyesha matumaini makubwa kwa Mangula na kuwa upo uwezekano mkubwa
wa CCM kuendelea kushinda kwa kishindo katika chaguzi
zake zijazo.
Baadhi
ya wananchi mashabiki wa vyama vya upinzani mjini Iringa walisema
kuwa CCM imetumia mbinu ya kunyong'onyeza nguvu ya vyama vya upinzani
katika jimbo hilo la Iringa mjini hasa chama cha Chadema ambacho
mbunge wake ni mchungaji Peter Msigwa .
Hivyo
walisema kuwa iwapo mbunge wa jimbo hilo Mchungaji Msigwa hatafanya
kazi zinazoonekana uwezekano wa kuambulia kura mwaka 2015 unaweza
kuwa mdogo japo walisema kuwa katika uchaguzi mkuu mwaka 2015
upinzani bado utategemea huruma za wana CCM kuendelea kumchagua mbunge
huyo ila iwapo CCM itafanya mchezo mchafu katika utaratibu wa kumpata
mgombea wa ubunge jimbo hilo.
Alisema
Damas Kalinga mkazi wa Kihesa ambaye alijitambulisha kuwa ni shabiki
wa Chadema kuwa hadi sasa ndani ya CCM jimbo la Iringa mjini tayari
wagombea wameanza kuwachanganya wananchi kwa kila mmoja kuonyesha
kuitaka nafasi ya ubunge na kuwataka viongozi wa CCM kuwa makini
zaidi.
Miongoni
mwa wabunge
waliojitokeza katika mapokezi hayo ni pamoja na mbunge wa viti
maalum mkoa wa Iringa Ritta kabati , mbunge wa jimbo la kalenga na
waziri wa fedha Dr Wiliam Mgimwa,makada wa CCM pamoja na wakuu wa
wilaya za Iringa , Kilolo na Mufindi wakiongozwa na mkuu wa mkoa wa
Iringa Dr Christine Ishengoma.
Kwa
upande wake mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa Jasca Msambatavangu
akimkaribisha Mangula katika uwanja
huo wa Mwembetogwa kwa
ajili ya kuwahotubia mamia ya wananchi waliofika katika uwanja
huo alisema kuwa CCM itaendelea kueleza utekelezaji wa Ilani ya
uchaguzi kwa wananchi wake na kuwa tayari baadhi ya kata zimeanza
kutoa utekelezaji wa ilani hiyo kwa wananchi.
Msambatavangu
aliwapongeza wanachama wa vyama vya upinzani ambao wameanza kurudi
CCM na kuwa kurejea kwa wanachama hao wa vyama
vya upinzani ndani ya CCM
ni kutokana na utekelezaji mzuri wa ilani yake kwa wananchi na
uendeshaji wa CCM ndani ya CCM bila kunadi sera za matusi na ubaguzi .
0 comments:
Post a Comment