Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo
(WAMA) Mama Salma Kikwete(kushoto) pamoja na Naibu wa Wizara ya Afya
Dkt.Seif Rashid (mwenye miwani) wakielekea kupanda ndege katika Uwanja
wa ndege wa kimataifa wa- JK- Nyerere jijini Dar es Salaam 16-jan 2013
kuelekea Arusha kwa ajili ya kufunga mkutano wa masuala ya Afya na Mtoto
jan. 17,2013. Mkutano huo unawashirikisha wajumbe wapatao 700 wa ndani
na nje ya nchi.
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na
Maendeleo(WAMA) Mama Salma Kikwete (mwenye kilemba) akisalimiana na
wafanyakazi wa ndani ya ndege katika Uwanja wa ndege wa kimataifa wa
Mwalimu JK Nyerere jijini Dar es Salaam Jan 16,2013 wakati akielekea
kufunga mkutano wa Masuala ya Afya na Mtoto hapo Jan 17,2013 mkoani
Arusha. Mkutano huo anawashirikisha wajumbe wapatao 700 wa ndani na nje
ya nchi, (kulia) ni Naibu Waziri wa Afya Dkt. Seif Rashid.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo Wanawake(WAMA)
kulia, Mama Salma Kikwete akizungumza na Mkuu wa Mkoa Arusha Magesa
Mulongo (kushoto) wakati alipowasil katika Uwanja wa ndege wa
kimataifa Kilimanjaro (KIA) Jan 16,2013
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo
(WAMA) Mama Salma Kikwete (kulia) akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya
Arusha John Mongela katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro
(KIA) Jan 16,2013.
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo
(WAMA) Mama Salma Kikwete(kulia) akiangalia vikundi vya sanaa ya ngoma
mbalimbali za utamaduni alipowasili katika kiwanja cha ndege cha
Kimataifa cha Kilimnjaro (KIA) jan 16.2013 kwaajili ya kufunga mkutano
wa masuala ya Afya ya Mama na Mtoto hapo Jan 17,2013 mkoani Arusha.
Aliengozana nae wapili ni Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake mkoa wa
Arusha (UWT) Flora Zelote
Kikundi cha kinamama cha ngoma ya Msanja kikitumbuiza katika
mapokezi ya Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na
Maendeleo (WAMA) Mama salma Kikwete (hayupo pichani) kwenye uwanja wa
ndege wa kimataifa Kilimanjaro (KIA ) Jan 16,2013.Picha na Mwanakombo Juma-MAELEZO
0 comments:
Post a Comment