- Mawaziri sita wameapishwa nchini Misri katika mabadiliko ya mwanzo ya baraza la mawaziri tangu katiba mpya kukubaliwa.
Serikali
sasa ina mawaziri wepya wa fedha na mashauri ya ndani ya nchi, wakati
serikali inajaribu kuimarisha uchumi uliozorota na sarafu iliyoporomoka.
Waziri
mpya wa fedha, El-Morsy El-Sayed Hegazy, amekariri kuwa Misri inataka
kukubaliana na IMF, ipewe mkopo wa dola bilioni nne na laki nane
milioni, ambao ulicheleweshwa kwa sababu ya msuko-suko wa kisiasa
nchini humo.
......XXXX........XXX.......XXX.......
Assad alaani wapinzani kuwa magaidi
Katika
hotuba yake ya mwanzo ya taifa tangu mwezi wa Juni, Rais Bashar
al-Assad wa Syria amelaani tena upinzani kuwa ni magaidi wanaosaidiwa
na mataifa ya nje, na alipendekeza ile aliyoita suluhu ya siasa ya
kumaliza vita.
Akihutubia
wafuasi waliomshangilia kwenye jumba la tamasha za opera mjini
Damascus, Rais Assad alieleza pendekezo lake la kuwa na mkutano wa
mapatano ya taifa ambao utaandika katiba mpya.
Lakini alisema hatazungumza na wale aliowaita karagosi wa mataifa ya Magharibi.
Kundi la upinzani la National Coalition in Syria, lilitoa maanani hotuba hiyo ya Rais Assad.
Msemaji wa NCS alinena kuwa rais anataka kuchafua makubaliano yoyote ya kimataifa ambayo yanaweza kumaliza utawala wake.
chanzo :BBC
0 comments:
Post a Comment