Waziri
wa Uchukuzi, Dk Harrison
Mwakyembe (kulia) akifafanua jambo kwa Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam
Waziri
wa
Uchukuzi, Dk Harrison
Mwakyembe (kulia) akifafanua jambo kwa Waandishi wa Habari jijini Dar
es Salaam leo wakati akitangaza maamuzi yaliyofikiwa na Bodi ya
Wakurugenzi juu ya
shutuma mbalimbali za Viongozi wa Bandari. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu
– Wizara ya Uchukuzi , John Mngodo na katikati ni Katibu Mkuu wa
Wizara ya Uchukuzi,
Mhandisi Omar Chambo.Picha Zote na Mdau Mroki.
WAZIRI wa Uchukuzi, Dk. Harrison
Mwakyembe, amewafukuza kazi vigogo watano wa Mamlaka ya Usimamizi wa
Bandari Tanzania (TPA) na kumrudisha mmoja kazini wakati mwingine
akifanyiwa uchunguzi upya.
Valiotimuliwa ni Mkuruganzi Mkuu wa TPA, Ephraim Mgawe, naibu wake
Hamad Konshuma, Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam, Casian Nghamilo,
Kapteni Tumaini Masalo na Julius Semfuko.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mwakyembe
alisema kuwa wanaendelea kumchunguza Kapten Lwakabale ambaye tuhuma
zake bado hazijabainika wazi.
Mwakyembe amefikia uamuzi huo kufuatia ripoti iliyotolewa na tume
ya uchunguzi iliyoundwa Agosti 27 mwaka jana, baada ya viongozi saba wa
mamlaka hiyo kusimamishwa kazi kutokana na tuhuma za ufisadi.
Alisema kuwa tume ilifanya kazi ya kuchunguza huduma mbalimbali za
bandari na kukabithi ripoti hiyo Oktoba mwaka jana. Vigogo hao
walikutwa na makosa ya uzembe uliokithiri, kushindwa kudhibiti wizi,
kukosa uaminifu kupindukia, matumizi mabaya ya madaraka na kukiuka
sheria.
Alisema kuwa makosa hayo yamesababisha kushindwa kudhibiti kiwango
cha utoaji mafuta machafu bandarini na kusababisha wizi wa mafuta
masafi pamoja na kutoa kibali cha utoaji mafuta hayo kinyume na sheria.
Waziri Mwakyembe aliongeza kuwa vigogo hao kwa kushirikiana
walitumia vibaya madaraka yao kwa kuingia mkataba na kampuni ya Kichina
(China Communication Construction Company) bila idhini ya serikali
pamoja na kupandisha mshahara kwa wafanyakazi wa bodi hiyo bila idhini
ya waziri anayesimamia mamlaka hiyo.
Alifafanua kuwa makosa hayo yote hayakuleta faida yoyote katika
kampuni hiyo zaidi ya kufukuza wateja na kusababisha hasara kubwa
ambayo mpaka sasa bado kiasi chake hakijajulikana.
Katika ripoti hiyo, Mwakyembe alisema kwa sasa bandari ya Dar es
Salaam ni ya mwisho kwa utendaji kati ya bandari 36 Afrika, kwa mujibu
wa utafiti uliofanywa na DANIDA na Benki ya Dunia.
Alisema kuwa uamuzi huo ni wa awali na tume bado inaendela kufanya
kazi yake. Na kuongeza kuwa amemrudisha kazini mhandisi Emmanuel Matala
baada ya kuona hana makosa.
Katika hatua nyingine, Mwakyembe alishindwa kubainisha ni hatua zipi kisheria zitafuata baada ya kuwafukuza kazi.
0 comments:
Post a Comment