Na Princess Asia
UTURUKI,
Uturuki, Uturuki, naam hizo ndizo zilikuwa shangwe za mashabiki wa Yanga leo
kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, baada ya kuifunga timu ngumu kutoka Afrika
Kusini, Black Leopard katika mchezo wa kirafiki.
Yanga iliyokuwa
kwenye kambi ya mafunzo nchini Uturuki kwa wiki mbili kabla ya kurejea Dar es
Salaam Jumapili iliyopita, imeibuka na ushindi wa mabao 3-2 jioni hii dhidi ya
timu hiyo inayoshirki Ligi Kuu ya Afrika Kusini.
Tegete, mfungaji wa mabao mawili ya Yanga leo |
Hadi mapumziko,
Yanga walikuwa mbele kwa bao 1-0 lililowekwa kimiani na mshambuliaji wake
aliyefufua makali, Jerry John Tegete dakika ya 33.
Tegete, alifunga
bao hilo kwa mkwaju wa penalti, baada ya kiungo wa kimataifa wa Rwanda, Haruna Hakizimana
Niyonzima kuangushwa kwenye eneo la hatari na beki Nkosiyaba Xakane na refa
Hashim Abdallah wa Dar es Salaam akatoa adhabu hiyo.
Kipindi cha
pili, kocha wa Yanga, Mholanzi Ernie Brandts alifanya mabadiliko, akiwatoa pacha
kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) wenye uraia wa Rwanda, Mbuyu
Twite na Kabange Twite na kipa Ally Mustafa ‘Barthez’ na kuwaingiza Simon Msuva,
Juma Abdul na kipa Said Mohamed.
Mabadiliko hayo,
hayakuisaidia Yanga, kwani Leopard walifanikiwa kusawazisha bao hilo dakika ya
kwanza tu tangu kuanza kipindi cha pili, lililofungwa kwa kichwa na Humphrey
Khoza aliyetumia udhaifu wa mabeki wa timu hiyo ya Jangwani na kumtungua kipa
Said Mohamed Kasarama.
Baada ya
kufungwa bao hilo, Yanga walicharuka na kufanikiwa kupata bao la pili dakika ya
63, lililofungwa na Frank Domayo aliyeunganisha krosi maridadi ya Niyonzima.
Jerry Tegete
aliifungia Yanga bao la tatu dakika ya 72 akiunganisha pasi ya beki Juma Abdul
na kuwafanya mashabiki wa timu hiyo waruke kwa shangwe za ‘Uturuki, Uturuki’,
kuashiria hayo ni matunda ya ziara ya timu hiyo nchini Uturuki kwa wiki mbili
zilizopita.
Beki Nadir Haroub
‘Cannavaro’ alimuangusha kwenye eneo la hatari Humphrey Khoza dakika ya 88 na refa akawapa penalti Leopard
ambayo ilikwamishwa kimiani na Rodney Romagalela na kufanya matokeo yawe 3-2.
Katika mchezo
huo, kikosi cha Yanga kilikuwa; Ally Mustafa ‘Barthez’/Said Mohamed dk 46,
Mbuyu Twite/Juma Abdul dk46, Oscar Joshua, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan,
Athumani Iddi ‘Chuji’, Kabange Twite/Simon Msuva dk 46, Frank Domayo, Jerry
Tegete, Didier Kavumbangu/Said Bahanuzi dk75 na Haruna Niyonzima.
AZAM YAPIGWA 2-1 IKISTAHILI KUSHINDA 3-2 KENYA
Mfungaji wa bao la Azam leo, Samih Hajji Nuhu akipongezwa na Mwaikimba |
Na Prince Akbar
AZAM FC
imeanza vibaya ziara yake ya Kenya, baada ya kufungwa mabao 2-1 kwa tabu na
wenyeji AFC Leopard katika mchezo wa kirafiki uliofanyika kwenye Uwanja wa
Nyayo, Nairobi, jioni hii.
Mabao ya
washindi katika mchezo huo, yalifungwa na Paul Were na Mike Barasa, wakati la
Azam lilifungwa na Sammih Hajji Nuhu kwa penalti.
Hata hivyo,
Azam itabidi wajilaumu wenyewe kupoteza mchezo huo, kwani walipoteza penalti mbili
kupitia kwa Joackins Atudo na Khamis Mcha ‘Vialli’.
Pamoja na
kufungwa, Azam ilionyesha soka maridadi jioni ya leo mjini hapa kiasi cha kuwavutia
mashabiki wa Kenya, waliojikuta wakiishangilia baada ya kuzimikia soka yao.
Katika mchezo
huo, kikosi cha Azam FC kilikuwa; Mwadini Ally, Himid Mao, Samir Hajji Nuhu,
Luckson Kakolaki, Joackins Atudo, Abdulhalim Humud/Ibrahim Mwaipopo, Jabir
Aiziz/Humphrey Mieno, Salum Abubakar/Kipre Balou, Gaudence Mwaikimba/Brian Umony,
Khamis Mcha na Uhuru Suleiman/Abdi Kassim ‘Babbi’.
chanzo: bin zuberry blog
0 comments:
Post a Comment