Watanzania wametakiwa kujenga mazoea ya kuwasaidia watoto
yatima badala ya kuwatumia kujipatia kipato au kuwadhulumu mali zao walizonazo ikiwemo zile
zilizoachwa na wazazi wao.
Rai hiyo imetolewa na diwani wa kata ya sokon one mh,
Michael kivuyo alipokuwa akiongea na wamiliki na walezi wa watoto yatima
waishio vituoni pamoja na watoto hao zaidi ya 100 kwenye ghafla fupi ya kupata
chakula cha mchana na watoto waishio katika vituo vya watoto yatima vilivyoko
katika kata ya sokon one.
Kivuyo amesema kuwa watu wengi kwa sasa hawana hata hofu ya
Kimungu kwani badala ya kuwasaidia watu wenye mahitaji kama yatima baadhi yao
wamekuwa wakiwatumia kujipatia kipato kwa kuanzisha vituo vya watoto yatima kwa
lengo la kujipatia kipato kutoka kwa wadau kwa madai ya kuwasaidia watoto hao
lakini kuhutumia misaada hiyo kwa manufaa yao binafsi.
Aliongeza kuwa si hao tu pia wako baadhi ya watu au hata
ndugu ambao wamekuwa wakiwanyanyasa watoto yatima walioachwa na wazazi wao
baada ya kutangulia mbele za haki kwa kuwanyanganya mali walizoachiwa na kujimilikisha
wao na kuwaacha watoto hao wakihangaika bila chochote wala msaada.
Mbali na hilo Kivuyo pia aliwageukia watoto hao yatima na
kuwataka watoto hao waliobahatika kuwepo kwenye vituo vya watoto yatima na
kulelewa vizuri hatimaye kuweza hata kusomeshwa wasijinyanyapae kuwa hawawezi
kufanya vizuri kwa kutokuwa na wazazi badala yake wajitahidi kufanya vizuri
katika masomo yao ili waweze kufaulu hatimaye kushika nafasi mbalimbali
serikalini au hata nafasi binafsi ili kuwasaidia wenzao baadae.
Kabla ya kuombea chakula hicho kilichoandaliwa na diwani kwa
ajili ya watoto yatima, mch, Julius Laizer alisisitiza kwa kuwataka watu kuwa
na hofu ya Mungu ya kuwadhulumu yatima na wajane mali zao badala yake wateke
baraka kwa kuwasaidia kuzitetea mali hizo na hata kujenga mazoea ya kutenga
bujeti zao na kuwasaidia watu hao ili
Mungu aweze kuwabariki na wao mara dufu.
Adha hafla hiyo iliyoandaliwa na familia ya diwani wa kata
ya sokon one ilifanyika katika kanisa la kipetekoste la Niavera iliyoka katika kata ya sokon one, ilihudhuriwa
na watoto yatima zaidi ya 100 waishio katika vituo 4 vya kata hiyo na wamiliki
wa vituo vya watoto hao wakiwemo walezi na wageni wengine.
0 comments:
Post a Comment