Watanzania wametakiwa kupunguza kuendekeza anasa na starehe kwa hali wanayotumia fedha nyingi
huko badala yake wawekeze kwenye elimu itakayoisaida taifa hapo baadae
kuondokana na changamoto mbalimbali zinazosababisha umaskini.
Rai hiyo imetolewa na kaimu mkurugenzi wa jiji la Arusha
Omary Mkombole, alipokuwa akihutubia kwenye maadhimisho ya miaka 50 ya shule ya
secondary Arusha iliyofanyika katika ukumbi wa shule hiyo.
Mkombole amesema kuwa watu wengi kwa sasa hudhani jukumu la
kusaidia mashule katika matatizo mbalimbali ikiwemo madawati na ukarabati na wa
majengo na vitabu ni jukumu la serikali tu hali ambayo si kweli bali jukumu ya
kuchangia katika elimu ni la kila mtu hivyo kila mtu ajitoe kuisaidai elimu
yetu isonge mbele.
Aidha aliongeza kuwa idadi kubwa ya watu kwa sasa hupenda
kutoa fedha zao nyingi zitumike kwenye anasa kama masherehe na kwenda kwenye
sehem za starehe na baadhi yao kujenga majengo makubwa ya mahoteli na mabaa tu
lakini huwa wagumu kujenga mashule na kuchangia katika kutatua kero zilizoko
mashuleni, hivyo kuwataka kuondoa mawazo hayo na mazoea hayo badala yake
wawekeze pia katika elimu kama kujenga mashule ili kuongeza hali ya kiwango cha
elimu mkoani hapa
Alisema kuwa anashangazwa na hali ya kisiasa iliyopo mkoani
hapa kwa baadhi ya watu kuendekeza maandamano ya majukwaani na kupoteza mda kwa
vitu visivyo na maana wala kuleta ukombozi wa nchi yetu hivyo kuwataka sasa
waandamane katika kuchangia elimu yetu ambayo ndio chanzo cha ukombozi wote wan
chi kwani kila mtu akielimika ukombozi huja bala hata maandamano.
Naye mkuuwa shule hiyo ya Arusha sekondari Christopha
Mallamsha katika kusima taarifa ya shule hiyo alisema kuwa ilianza rasmi mwaka
1962 ikiwa na wanafunzi 289na sasa ina wanafunzi zaidi ya 2000 ambapo hadi leo
inaapoadhimisha miaka 50 wameshahitimu wanafunzi wengi huku baadhi yao wakiwa ni viongozi wenye nyadhfa mbalimbali kama wabunge, mawaziri, wakuu wa mikoa, wakuu wa wilayana
wataalam mbalimbali.
Akitaja matatizo yanayoikabili shule hiyo alisema kuwa ni
eneo la shule walilonyanganywa na wananchi kwa madai ni eneo lao, pia ukosefu
wa baabara na maktaba pia uzio wa upande wa chini wa shule hiyo ambapo
amemuaomba mkurugenzi kushughulikia swala hilo ili kudumisha kiwango cha elimu
shuleni hapo.
Sambamba na maadhimisho hayo pia iliambatana na harambee
fupi ya kuchangia jengo la maktaba ambapo walifanikiwa kuchanga zaidi ya
milioni 33 huku jiji likichangia shilingi milioni 5.
.
0 comments:
Post a Comment