Wakazi wa mji mdogo wa Dumila Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro
wakiwakimbia askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) katika
barabara ya Dodoma-Morogoro juzi. Picha na Juma Mtanda
WATU wanane wameuawa na wengine kumi na moja kujeruhiwa
kutokana na vurugu zilizizotokea jana mkoani Mtwara na Itete wilayani
Ulanga, mkoani Mororgoro.
Muuguzi
wa zamu katika Hospitali ya Wilaya ya Masasi, Mkomaindo, Amima Simbo
alithibitisha vifo vya watu saba waliofikishwa hospitalini hapo.
Kwa
mujibu wa muuguzi huyo, maiti zilizopokelewa hospitalini hapo
zilionekana zikiwa na matundu yanayodhaniwa kuwa ni ya risasi, baadhi
yao kichwani, begani, viunoni na tumboni.
Aidha majeruhi waliofikishwa hospitalini hapo pia walikuwa na majeraha mbalimbali ikiwamo ya risari.
Habari
zaidi zinaeleza kuwa vurugu hizo zilizuka baada ya kundi la waandamaji,
wengi wakiwa vijana waendesha pikipiki maarufu kama bodaboda waliokuwa
wakipinga mwenzao kukamatwa na kutaka kuvamia Kituo cha Polisi ili
kumwokoa.
Vurugu
hizo ziliendelea kuutikisa Mkoa wa Mtwara kwa siku ya pili mfululizo na
kuutikisa Mkoa wa Mtwara, baada ya vurugu nyingine kuibuka wilayani
Masasi jana.
Habari
zinasema mbali na vifo na majeruhi, nyumba za wabunge wawili wa wilaya
hiyo zimechomwa moto, ambapo pia magari, trekta, Ofisi za CCM Wilaya na
Ofisi ya Mkurugenzi wa Wilaya ziliharibiwa kwa kuchomwa moto.
Wabunge ambao nyumba zao zimemwa moto ni Mariam Kasembe wa Masasi Mjini na Anna Abdallah Mbunge wa Viti Maalumu wilayani humo.
Juzi
vurugu hizo zilitokea katika Mikoa ya Morogoro kati ya wakulima na
wafugaji na kusababisha kifo cha mtu mmoja wakati mkoani Mtwara
wananchi wa eneo la Chikongola waliizingira nyumba ya diwani wa Kata
ya Mikindani, Mohamedi Chehako kwa madai ya kuwahifadhi wachawi ndani
ya nyumba yake.
Katika
vurugu hizo polisi walilazimika kutumia silaha yakiwamo mabomu ya
machozi ili kupoza hali ya hewa, ambapo nyumba ya Waziri wa Nchi Ofisi
ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Hawa
Ghasia ilichomwa moto.
Akizungumza
na Mwananchi Jumapili kuhusu vurugu hizo, Mbunge wa Masasi Mjini,
Mariam Kasembe alisema kuwa nyumba yake iliyoko Masasi mjini imechomwa
moto na kuteketea kabisa, huku mali zikiibwa na kwamba familia yake
sasa haina makazi.
Aliongeza kwamba mbali na uharibifu, vurugu hizo zimesababisha pia mama yake mzazi kukimbia na mpaka sasa hajulikani alipo.
“Wamechoma
trekta na gari lililokuwepo nyumbani kwangu, watoto wangu na mume wangu
walipoona hali hiyo wakakimbia,” alisema Kasembe akieleza kuwa hawezi
kuthibitisha chanzo cha vurugu hizo, lakini anahisi kuwa zinatokana na
mgogoro wa gesi.
0 comments:
Post a Comment