Imebainika kuwa uroho wa mali na ngombe kwa baadhi ya
wanajamii ya wamasai imekuwa chanzo cha uonevu na unyanyasaji wa watoto wa wa
kike huku mfumo dume ukishika kasi kwa jamii hizo na mwanamke kuonekana na kama
chanzo cha mali hizo.
Hayo yamebeinika na mwandishi wa habari hizi alipotembelea
katika kata ya Mateves iliyoko wilayani Arumeru Mkoani Arusha na kukutana na
binti wa jamii ya kimasai anayeiomba serikali kuwasaidia watoto wa kike hasa wa
jamii ya hiyo kwani wamekuwa wakinyanyaswa na baba na kaka zao kuwa mtoto wa
kike hana haki ya kusoma bali kuolewa na kuongeza mali nyumbani ambayo ni
mifugo ikiwemo ngombe
Akiongea na kipindi hiki huku akitokwa na mchozi msichana
Namnyaki Loishiye (17) mkazi wa kata ya mateves amefikia hatua ya kuiomba
serikali kuwasaidia haki ya kupata elimu watoto wa kike kwani wamekuwa
wakinyanyaswa sana ambapo yeye alilazimishwa kuolewa na baba yake aliyejulikana
kama Loishiye Lesengere akiwa darasa la 6 na umri wa miaka 14 na kupokea mahari
kutoka kwa Loihorwa Sindiyo.
Aidha amesema kuwa baada ya kukataa na kupigwa sana
aliwaomba wazazi wake wamunvumilie amalize darasa la saba ambapo alipomaliza
mwaka jana baba yake alifariki lakini alikuja kuibwa asubuhi ya pili yake na m,wanaume
aliyelipa mahari na kwenda kuolewa lakini baada ya kukaa wiki tatu mama yake
alikwenda kushitaki polisi na kurudishwa nyumbani lakini bado uwezo wa
kuhudumiwa mahitaji shule ni ngumu hivyo kuiomba serikali ya wilaya mkoa kwa
ujumla kumsaidia ili aweze kutimiza ndoto zake za kuwa mwalim.
Msichana Namnyaki alikuwa anasoma katika shule ya msingi
Lenjoro iliyoko wilayani Arumeru katika kata ya Mateves Na kumaliza elimu yake
ya msingi mwaka jana 212 na kufanikiwa kufaulu kwenda katika shule ya sekondari
Oljoro ambapo alitoroshwa na kwenda kuolewa lakini sasa amerudi ila pamoja na
kurudi nyumbani bado matumaini ya kusoma na kutimiza ndoto zake za kuwa mwalim
ni hadithi hivyo serikali na jamii nzima kilio hiki kinawaangukia kujitokeza
kuweza kumsaidia
0 comments:
Post a Comment