Timu
ya Young Africans Sports Club kesho alfajiri inatarajiwa kusafiri
kuelekea jijini Mwanza ambapo siku ya jumatano itacheza mchezo wa
kirafiki wa marudiano dhidi ya timu ya Black leopard kutoka nchini
Afrika Kusini katika Uwanja wa CCM Kirumba.
Mchezo
huo wa jumatano utakua ni fursa kwa wakazi, wapenzi wa soka wa kanda ya
ziwa kuweza kuiona timu yao kwani tangu irejee nchini kutoka Uturuki
imecheza mchezo mmoja tu wa kirafiki katika Uwanja wa Taifa jijini Dar
es salaam, hivyo ni fursa nzuri kwa wapenzi wa soka kanda ziwa kuiona
timu yao.
Katika
mchezo wa kwanza Young Africans iliibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi
ya Black leopard huku mabao ya Yanga yakifungwa na Jerson Tegete mabao
mawili na Frank Domayo akifunga bao moja na pia kuchaguliwa kuwa
mchezaji bora wa mechi hiyo.
Kocha
Mkuu Ernest aliomba kupata michezo miwili ya kirafiki kabla ya kuanza
kwa mzunguko wa pili wa ligi kuu ya Vodacom ambayo inatarajiwa kuanza
kutimua vumbi mwishoni mwa wikii hii katika viwanja tofauti, Yanga
ikianza na timu ya Prisons siku ya jumapili.
Aidha
Black Leopard ambayo iko nchini Tanzania kwa ajili ya maandalizi ya
mzunguko wa pili wa ligi kuu nchini Afrika kusini PSL imesifia mchezo
wa juzi dhidi ya Yanga na kusema ulikuwa mchezo mzuri na wakuvutia
japokuwa walifungwa, lakini watajitahid kupata ushindi katika mchezo
wao wa marudiano siku ya jumamosi.
Young
Africans ambayo itatumia mchezo huo kama maandalizi yake ya mwisho,
itaondoka kesho alfajiri na msafara wa watu 37, wachezaji 27, benchi la
ufundi 7 na viongozi 3.
Timu
itarejea Dar es salaam siku ya alhamis jion tayari kabisa kwa kujiandaa
na mchezo wa kwanza wa mzunguko wa pili wa ligi Kuu ya Vodacpm dhidi ya
timu ya Prisons ya Mbeya.
Kuhusu viingilo vya mchezo huo ni vitakua ni Jukwaa Kuu Tshs 10,000/=, na mzunguko Tshs 3,500/=
0 comments:
Post a Comment