.

.
Sunday, December 9, 2012

1:09 AM
John Bocco
Na Mahmoud Zubeiry
AJABU na kweli. Robert Ssentongo amepewa tuzo ya ufungaji  wa Kombe la Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge jana, wakati anazidiwa mabao na washambuliaji wa Tanzania Bara, John Raphael Bocco na Mrisho Khalfan Ngassa, ambao kila mmoja ana mabao matano.
Ssentongo amemaliza mabao manne, lakini jana CECAFA ikampa tuzo hiyo na kuwaacha wengi midomo wazi. 
Uganda ilitwaa Kombe la Chalenge jana kwa kuifunga Kenya mabao 2-1, ambayo yote Kenya walijfunga jana kupitia kwa wachezaj wao Anthony Kimani na Joackins Atudo. Bao la Kenya lilifungwa na Edwin Lavatsa.
Mbali na Ngassa na Bocco kuongoza wakifuatiwa na Ssentongo, wengine waliokuwamo kwenye kinyang’anyiro ni Brian Umony wa Uganda aliyemaliza na mabao matatu, sawa Khamis Mcha ‘Vialli’ wa Zanzibar, Suleiman Ndikumana na Chris Nduwarugira wa Burundi.
Wachezaji wenye mabao mawili kila mmoja ni Geoffrey Kizito wa Uganda, David Ochieng, Mike Barasa, Clifton Miheso wa Kenya na Dadi Birori wa Rwanda.
WAFUNGAJI CECAFA TUSKER CHALLENGE 2012
John Bocco                   Tanzania 5
Mrisho Ngassa              Tanzania 5
Robert Ssentongo         Uganda   4
Brian Umony                 Uganda   3
Khamis Mcha                Zanzibar  3
Suleiman Ndikumana    Burundi   3 (1 penalti)
Chris Nduwarugira        Burundi   3
Geoffrey Kizito              Uganda   2
David Ochieng              Kenya      2
Clifton Miheso               Kenya      2
Dadi Birori                     Rwanda   2
Mike Barasa                  Kenya      2

0 comments:

Post a Comment