.

.
Saturday, December 8, 2012

12:27 PM
Ngassa
Na Mahmoud Zubeiry
WAKATI Kombe la Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge, linafikia tamati leo mjini Kampala, Uganda ushindani mkubwa umeibuka katika kinyang’anyiro cha ufungaji bora wa mashindano hayo yaliyoanza Novemba 24, mwaka huu mjini hapa.
Washambuliaji wa Tanzania Bara, John Raphael Bocco na Mrisho Khalfan Ngassa hadi sasa waongoza, kila mmoja akiwa na mabao matano, wakifuatiwa na Robert Ssentongo wa Uganda, mwenye mabao manne. 
Uganda leo itamenyana na Kenya katika fainali na Ssentongo atakuwa na nafasi nyingine ya kufunga, wakati Bara itamenyana na Zanzibar kusaka nafasi ya tatu na Ngassa na Bocco pia watakuwa na nafasi ya kuongeza mabao pia.
Lakini pia watatu hao wote wanaweza kuikosa tuzo hiyo, iwapo wachezaji wengine wenye mabao matatu watafunga idadi kubwa ya mabao katika mechi za leo na wao wakatoka kapa.
Hao ni Brian Umony wa Uganda mwenye mabao matatu, sawa Khamis Mcha ‘Vialli’ wa Zanzibar. Suleiman Ndikumana na Chris Nduwarugira wa Burundi, nao pia wana mabao matatu kila mmoja, lakini timu yao imekwishatolewa.
Wachezaji wenye mabao mawili kila mmoja ni Geoffrey Kizito wa Uganda, David Ochieng, Mike Barasa, Clifton Miheso wa Kenya na Dadi Birori wa Rwanda, ambao timu yao imekwishatolewa.
WAFUNGAJI CECAFA TUSKER CHALLENGE 2012
John Bocco                    Tanzania 5
Mrisho Ngassa               Tanzania 5
Robert Ssentongo          Uganda    4
Brian Umony                  Uganda    3
Khamis Mcha                 Zanzibar  3
Suleiman Ndikumana     Burundi   3 (1 penalti)
Chris Nduwarugira        Burundi   3
Geoffrey Kizito              Uganda    2
David Ochieng               Kenya       2
Clifton Miheso               Kenya       2
Dadi Birori                      Rwanda   2
Mike Barasa                   Kenya       2

0 comments:

Post a Comment