.

.
Monday, December 10, 2012

10:59 PM
nnnnnn -->
kutoka kushoto ni katibu kata ya Monduli, na anayefuata ni mkuu wa wilaya ya Monduli Jowika Kasunga na mwingine ni Diwani wa kata ya Moita Edward Sapunyo (aliyesimama) na mwisho ni Afisa elimu msingi wilaya ya Monduli katika kikao cha kutathmini hali ya kielimu wilayani Monduli Mkoani Arusha nchini Tanzania

 Imebainika kuwa mila na desturi hasa kwa jamii ya kimasai  bado ni changamoto kubwa inayofanya kushuka kwa kiwango cha elimu wilayani Monduli mkoani Arusha

mratibu elimu kata ya Moita wilayani Monduli bwana Swati alipokuwa akisoma taarifa ya hali ya elimu katika kata hiyo tangu mwaka 2007 hadi 2012 mwaka huu

     
-->Akisoma taarifa ya hali taaluma katika kata ya Moita iliyoko katika halmashauri ya wilaya ya Monduli, mratibu elimu kata  alisema kuwa mila na desturi hasa za tohara kwa watoto wa kike na kiume imekuwa chanzo cha watoto wengi kutokumaliza shule kwa kujiona wameshakua.

Akifafanua kwa watoto wa kike alisema kuwa baadhi ya watoto wa kike wakishafanyiwa tohara hujiona ni mtu mzima na  kuona elimu haina maana kwake badala yake huenda kuolewa kwa kufuata msukumo wa wazazi wake na kuacha shule.

 Aidha kwa watoto wa kiume wakishafanyiwa tohara hujiona ni watu wazima hivyo hudharau walimu hasa wa kike na pia kutotaka kujichanganya na wengine  wasiotahiriwa hali ambyo mazingira ya shule humshinda na kuamua kuacha na kwenda kuchunga ngombe za wazazi wao kutokana na shuleni hakuna sheria za kuwatenga waliotahiriwa na wasiotahiriwa.

Aliongeza kuwa hali hiyo pia huungwa mkono na wazazi wao hali aambayo imekuwa usumbufu mkubwa kwa baadhi ya walimu pamoja na maafisa elimu pindi wakiwafuatilia nyumbani kwao.

baadhi ya watu waliohudhuria kwenye kikao hicho wakiwemo wanahabari Deo Macha na Kessy Lukumai

-->
Kwa upande wake aliyekuwa mgeni rasmi katika kikao hicho, mkuu wa wilaya ya Monduli, Jowika Kasunga aliwataka walimu wa shule za sekondari na misingi zilizoko katika kata ya Moita kutokuwafanya wanafunzi wanaowafundisha kama watumwa wa mapenzi badala yake wawafundishe na kuwachukua kama watoto wao.

Kasunga alisema kuwa baadhi wa walimu hasa wa kiume wamekuwa na tabia ya kuwarubuni watoto wa kike na kujenga nao mahusiano ya kimapenzi huku kwa baadhi ya walimu wa kike huhalalisha baadhi ya watoto kwenda kuolewa kwa kuhongwa hela na waoaji hali ambayo hufanya mahudhirio ya watoto hao kuwa duni na baadae kuacha shule.

Kasunga pia amewataka walim hao kuona matatizo ya wanafunzi kama matatizo yao kwani kasoro mbalimbali zinazojitokeza kwa walimu ndizo zinazowakumba na wanafunzi ikiwemo mwalimu kutimiza majukumu yake kwa zaidi ya asilimia 50 ambapo wanafunzi nao humaliza shule wakiwa hawajui hata kusoma wala kuandika na kwa baadhi ya watoto wa jamii ya kimasai baadhi humaliza hawajui hata lugha ya Kiswahili wala kuandika jina lake.

Kutokana na mwenendo huo mkuu huyo aliwatahadharisha walimu hao kuwa endapo fani ya ualimu inawashinda basi ni bora wakatafute shughuli zingine za kufanya kama ujasiriamali, ubaamedi au hata biashara nyingine kuliko kuendelea kudidimiza elimu katika kata hiyo la sivyo watachukuliwa hatua kali za kisheria.

 Aidha kikao hicho kiliwahusisha viongozi wa ngazi zote za kata hiyo, maafisa elimu wa shule za misingi na sekondari pamoja na walimu wanaofundisha shule za misingi na sekondari zilizoko katika kata hiyo ya Moita wilayani monduli mkoani Arusha.
baadhi ya watu waliohudhuria kikao hicho

0 comments:

Post a Comment