.

.
Friday, December 7, 2012

11:14 AM

 Na Joseph Ngilisho -Arusha
Mwanafunzi wa darasa la tatu katika shule ya msingi Sombetini mwenye umri wa miaka 10 (jina limehifadhiwa) jijini Arusha,amelazwa katika hospital ya mkoa Mount Meru baada ya kubakwa na kuharibiwa vibaya sehemu zake za siri na mwanaume mwenye umri wa miaka 40 ambaye ni mtoto wa diwani.
Akizungumza na vyombo vya habari mama mdogo wa mtoto huyo ,Fatuma Zuberi alisema kuwa tukio hilo ambalo limethibitishwa na jeshi la polisi jijini hapa,limetokea novemba 30 mwaka huu majira ya saa moja jioni  nyumbani kwao mtaa wa Pangani jijini hapa.
Akisimulia zaidi alisema kuwa siku ya tukio yeye na familia hapo nyumbani walienda kwenye sherehe za kicheni pati na kumwacha mtoto huyo nyumbani akiwa na bibi yake.
Alisema kuwa baada ya kutoka katika sherehe hiyo majira ya saa 4 usiku walimkuta mtoto huyo  akiwa amelala chumbani bila kuwa na nguo ya ndani na kumhoji ,hata hivyo mtoto huyo alisema kuwa hakuvaa chupi kwa kuwa ilikuwa inambana.
Alieleza kuwa alimwamuru mtoto asilale bila kuvaa nguo ya ndani na kumtaka achukue nguo hiyo avae ,hata hivyo alipigwa na butwa baada ya kuona nguo hiyo ikiwa mbichi imetapakaa mbegu za kiume na damu, ndipo aliposhtuka na kutaka kumwadhibu mtoto huyo,kutokana na mtoto huyo kutotaka kueleza kilichotokea.
Aliongeza kuwa aliamua kumchapa ndippo aliposema ukweli kwamba alibakwa na mwanaume aliyemtaja kwa jina la Thabit Jafari(40) ambaye ni jirani yao na ni mtoto wa diwani wa kata ya mjini  kati(ccm),Abdulrasul Tojo.
‘’tulishangaa baada ya kuelezwa kuwa Jafari ndiye aliyehusika kumbaka mtoto wetu hatukuamini kwani kijana huyo ni jirani yetu na tumekuwa tukiishi naye kwa muda mrefu kama ndugu na kwamba huyo anafamilia yake na anamtoto wa kike anayesoma kidato cha tatu’’alisema Fatuma.
Alisema kuwa baada ya tukio hilo waliamua kumpigia simu kijana huyo na ndipo alipokiri na kueleza kuwa alifanya tukio hilo baada ya kupitiwa na shetani na kuomba wamsamehe na kwamba hatorudia tena tukio kama hilo.
Hata hivyo hawakuridhika na maelezo ya kijana huyo kutokana na kuelezwa na mtoto huyo kwamba, tukio hilo halikuwa la kwanza kutokea kwani amekuwa akimfanyika tendo hilo mara kwa mara na mara nyingi  humfanya majira ya usiku wakati mtoto anapoenda kuosha vyombo.
Familia ya mtoto huyo iliamua kutoa taarifa polisi baada ya kumweleza baba wa mtuhumiwa ambaye ni diwani wa kata ya mjini kati, na kushindwa kuwapa ushirikiano ambapo walifika kituo cha polisi mjini kati na kufungua

0 comments:

Post a Comment