.

.
Monday, December 3, 2012

2:06 PM

KIJANA mmoja aliyetambulika kwa jina moja la Abdul mwenye umri wa miaka 20, Mkazi wa Ilboru jijini Arusha, anatuhumiwa kumbaka mtoto wa miaka miwili.
Kwa mujibu wa mashuhuda, Abdul, mkazi, mapema leo hii (dec 3), alimwita chumbani mwake mtoto wa mpangaji mwenzake (jina tunalihifadi) na kisha akamfanyia kitendo hicho cha kinyama.
Wapangaji wenzake waliposhtukia tukio hilo la ubakaji, walivamia chumba chake na kumshushia kipigo kikali kabla ya kumpeleka kituo kikuu cha polisi,Jijini Arusha.
Mtoa habari wetu alisema mtuhumiwa alipohojiwa na polisi alikiri kuwa ni kweli alimbaka mtoto huyo kwa kisingizio eti alipitiwa na shetani.
Hata hivyo majirani wa Abdul wanasema hiyo imekuwa ni kawaida yake kujihusisha na vitendo vinavyohusiana na ubakaji na tayari ana kesi nyingine makahamani kwa tuhuma hizo hizo za ubakaji.
Saluti5 ilifanikiwa kufanya mahojiano na mama mzazi wa mtoto huyo aliyejitambulisha kwa jina la Mariam akiwa ndani ya wodi namba 9 katika hospitali ya mkoa (Mount Meru) ambapo alikiri binti yake kufanyiwa ubakaji na mpangaji mwenzake.
Akiongea huku akitokwa na machozi pembeni ya kitanda alicholazwa mwanae, Mariam alisema bado hajajua hatma ya afya ya mwanae 

0 comments:

Post a Comment