.

.
Tuesday, December 18, 2012

10:53 PM
Haya siyo mashimo ya taka wala visima vya maji vilivyokauka bali ni barabara ya treni (reli) iliyoko mkoni Arusha kata ya daraja mbili jijini Arusha vinavyotumika hadi leo hii kwa usafirishaji wa binadam na mizigo bila kuhofia upenyo huo,

Ajali ikitokea eneo hilo nani wa kulaumiwa kwani reli hiyo iko karibu kabisa na ofisi ya kata ya daraja mbili ambao ndio wahusika (viongozi) wasije sema hawakujua ajali ikitokea hivyo basi warekebishe,

Mkuu wa mkoa wa A rusha Magessa Mulongo na mkuu wa wilaya ya Arusha John Mongela wanaweza sema hawakuona kwani hawakutembelea eneo hilo siku ajali ikitokea na kusababisha ndugu zetu kupoteza maisha hivyo basi waone kupitia hapa kusiwepo kisingizio (heri kinga kuliko tiba)

karibu na reli hiyo kunaofisi ya kata ya daraja mbili inayoongozwa na diwani wake Prosper Msofe na kata hiyo iko chini ya jiji la Arusha inayoongozwa na mkurugenzi wake Omary Mkombole, chukueni hatua haraka hasa msimu huu wa sikukuu watu wanasafiri kutoka eneo moja kwenda lingine hivyo hata Arusha wanakuja wengine kupitia reli hiyo.



0 comments:

Post a Comment