.

.
Sunday, December 2, 2012

1:59 PM

Ngassa akibusu mpira jana

Na Mahmoud Zubeiry, Kampala
MSHAMBULIAJI wa Tanzania Bara, Mrisho Khalfan Ngassa amesema kwamba pamoja na kuongoza kwa mabao katika Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge lakini atafurahi hata kama mfungaji bora akiwa mchezaji mwenzake wa Kilimanjaro Stars, John Bocco ‘Adebayor’.
Ngassa anaongoza kwa mabao yake matano, aliyofunga katika mechi moja tu dihidi ya Somalia jana, wakati Bocco ana mabao manne, aliyofunga mawili kila mechi dhidi ya Sudan na jana na Wasomali.
Akizungumza na BIN ZUBEIRY baada ya mechi ya jana, Ngassa alisema kwamba yeye kama mchezaji anaweka mbele maslahi ya timu hivyo mfungaji bora akiwa yeyote baina yake na Bocco atafurahi.
“Siku zote mimi napocheza huwa naweka mbele maslahi ya timu, ndiyo maana ukifuatilia rekodi yangu kuanzia kwenye Ligi Kuu, mimi ndiye mchezaji ninayeongoza kutoa pasi za mabao,”alisema Ngassa. 
Jumla ya mabao 44 hadi sasa yamefungwa katika mechi 24 za kwenye hatua ya makundi pekee tangu kuanza kwa mashindano haya Novemba 24.
Wakati Ngassa anaongoza kwa mabao yake matano, akifuatiwa na Bocco wa Azam FC mwenye manne, nafasi ya tatu wanafungana Suleiman Ndikumana wa Burundi mwenye mabao matatu, moja la penalti, Brian Umony wa Uganda na Chris Nduwarugira wa Burundi pia.
Wanaofuatia ni Khamis Mcha ‘Vialli’ wa Zanzibar mwenye mabao mawili sawa na David Ochieng na Clifton Miheso, wote wa Kenya.
Waliofunga bao moja kila mmoja katika mashindano haya ni Yussuf Ndikumana wa Burundi, Mohamed Jabril wa Somalia kwa penalti, Geoffrey Kizito, Hamisi Kiiza, Robert Ssentongo wote wa Uganda Yonatal Teklemariam wa Ethiopia, Haruna Niyonzima, Jean Mugiraneza, Dadi Birori, Tadi Etikiama na Tumaine Ntamuhanga, wote wa Rwanda.
Wengine wenye bao moja kila mmoja ni Ramadhan Salim wa Kenya, Gatech Panom Yietch wa Ethiopia, Farid Mohamed wa Sudan, Chiukepo Msowoya, Miciam Mhone, Patrick Masanjala, wote wa Malawi, Amir Hamad Omary na Yosief Ghide kwa penalti, wote wa Eritrea. 


WAFUNGAJI CECAFA TUSKER CHALLENGE 2012
Mrisho Ngassa               Tanzania  5
John Bocco                    Tanzania  4
Suleiman Ndikumana     Burundi    3 (1 penalti)
Brian Umony                  Uganda    3
Chris Nduwarugira         Burundi    3
Khamis Mcha                 Zanzibar   2
David Ochieng               Kenya       2
Clifton Miheso                Kenya       2
Yussuf Ndikumana        Burundi     1
Mohamed Jabril             Somalia    1(penalti).
Geoffrey Kizito               Uganda    1
Hamisi Kiiza                   Uganda    1
Robert Ssentongo          Uganda    1
Yonatal Teklemariam     Ethiopia    1
Haruna Niyonzima         Rwanda    1
Jean Mugiraneza           Rwanda    1
Dadi Birori                     Rwanda    1
Tadi Etikiama                 Rwanda    1                     
Tumaine Ntamuhanga   Rwanda    1
Ramadhan Salim           Kenya       1
Gatech Panom Yietch    Ethiopia    1
Farid Mohamed              Sudan       1
Chiukepo Msowoya        Malawi       1
Miciam Mhone                Malawi      1
Patrick Masanjala           Malawi      1
Amir Hamad Omary       Eritrea        1
Yosief Ghide                 Eritrea       1(penalti).

0 comments:

Post a Comment