.

.
Saturday, December 29, 2012

12:11 PM

TUSKER TATU, SIMBA TILA LILA TAIFA

Tusker wakishangilia mbele ya mashabiki wa Simba 

Na Mahmoud Zubeiry
SIMBA SC imefungwa mabao 3-0 na Tusker ya Kenya katika mchezo wa kirafiki uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Katika mchezo huo, uliochezeshwa vema na refa Hashim Abdallah, hadi mapumziko, tayari Tusker walikuwa mbele kwa mabao 2-0, yaliyotiwa kimiani na Jesse Were dakika ya 37 na 45.
Mabao yote yalitokana na udhaifu wa safu ya ulinzi ya Simba, ambayo hii leo iliongozwa na beki kutoka Mali, Komabil Keita kiasi cha kufikia mfungaji anafunga akiwa amebaki anatazamana na kipa.
Simba ilikuwa ikishambulia kutokea pembeni, lakini mipira mingi mirefu iliyokuwa inamiminwa langoni mwa Tusker ilikuwa inaokolewa na mabeki warefu wa klabu hiyo bingwa ya Kenya, wakiongozwa na beki wa zamani wa Yanga, Joseph Shikokoti.
Kipindi cha pili, Tusker walirudi kwa nguvu tena na kufanikiwa kupata bao la tatu dakika ya 54, mfungaji Frederick Onyango.
Simba pamoja na kufanya mabadiliko, ikiwatoa Haruna Shamte, Haruna Athumani, Paul Ngalema, Mussa Mudde, Abdallah Seseme, Abdallah Juma, Ramadhani Chombo na Kiggi Makassy na kuwaingiza Miraj Adam, Hassan Isihaka, Emily Ngeta, Jonas Mkude, Salim Kinje, Haruna Moshi, Ramadhani Singano, Nassor Masoud ‘Chollo’ na Edward Christopher, haikuweza kupata hata bao la kufutia machozi.
Nassor Masoud aliingia kuchukua nafasi ya Shamte, lakini naye akaumia na kutoka nafasi yake ikichukuliwa na kinda wa Simba, B, Masele Kaheza.
Simba SC; William Mweta, Haruna Shamte, Paul Ngalema, Hassan Khatibu, Komabil Keita, Mussa Mude, Haroun Athumani, Abdallah Seseme, Abdallah Juma, Ramadhan Chombo na Kiggi Makassy.
Tusker FC; Samuel Odhiambo, Luke Ochieng, Jeremiah Bright, Mark Odhiambo, Joseph Shikokoti, Khalid Aucho, Edwin Manono, Frederick Onyango, Ismail Dunga, Jesse Were, Robert Omonuk,  
Mshambuliaji wa Simba SC, Abdallah Juma akijaribu kumtoka beki wa Tusker ya Kenya, Frederick Onyango katika mchezo wa kirafiki jioni hii Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Tusker ilishinda 3-0. 

Beki wa Tusker, Joseph Shikokoti akikabiliana na kiungo wa Simba Abdallah Seseme kushoto 

Seseme akimiliki mpira mbele ya kiungo wa Tusker

Haruna Athumani akitafuta mbonu za kumtoka beki wa Tusker, Onyango

Jeremiah Bright wa Tusker akimdhibiti Mussa Mudde wa Simba

Haruna Shamte akiosha

Haruna Athumani akikabiliana na beki wa Tusker, Edwin Ombassa

Kiggi makassy akimdhibiti Jesse Were

Mudde akitafuta njia

Shikokoti ameruka hewani kupiga kichwa peke yake

Shikokoti akimiliki mpira mbele ya kiungo wa Simba, Haruna Athumani

0 comments:

Post a Comment