.

.
Wednesday, December 5, 2012

9:48 PM

270 wafariki katika kimbunga Ufilipino



Athari za kimbunga Bhopal nchini Ufilipino

Zaidi ya watu mia mbili sabini wamethibitishwa kufariki katika kimbunga kikali kinachoendelea kusababisha uharibifu kusini mwa Ufilipino.
Wengine wengi hawajulikani waliko. Nusu ya walioathiriwa walikuwa ni wakaazi katika maeneo ya milima walioathirika na maporomoka ya udongo baada ya kuyakimbia makaazi yao ili kwenda kwenye maeneo yalio salama.
Katibu mkuu wa shirika la msalaba mwekundu nchini humo, Gwendolin Paang, ameiambia BBC kuwa idadi ya waliofariki inatarajiwa kuongezeka.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka shirika la AP Miili zaidi ya 270 ya watu waliofariki katika kimbunga hicho ilipokelewa katika maeneo yalioathiriwa na kimbunga hicho kusini mwa ufilipino.
Kwa mujibu wa maafisa nchini humo huenda miili zaidi ikapatikana katika maeneo mengine ambayo kwa sasa waokoaji wanaendeleza shughuli za uokozi.
Katika mkoa wa Compostela zaidi ya watu 151 wakiwemo wanajeshi na wenyeji wameripotiwa kufariki katika mafuriko yaliyosababishwa na kimbunga hichi cha bopha .
Zaidi ya watu 80 waliponea kimbunga hicho lakini wengi bado hawajulikani walipo na wengine zaidi ya elfu 45 wakikosa makao.
Idadi ya vifo hivi vimetokea licha ya rais wa ufilipino Benigno Aquino kutaka raia wa ufilipino kuhamia maeneo yaliyo salama. Nchi ya ufilipino hukumbwa na zaidi ya vimbunga 20 kila mwaka.
                             .........XXX............XXX............XXX...........

Wanajeshi 12 wa Somalia wauawa na Al Shabaab


Wapiganaji wa Al Shabaab sasa wametorokea Kusini mwa Somalia

Maafisa kutoka jimbo lililojitenga la Puntland nchini Somalia wamesema kuwa wanajeshi kumi na mbili wa serikali ya Somalia wameuwawa na kundi la wanamgambo wa kislaamu la Al shabaab katika eneo la milima ya Galgalo
Walisema kulikuwa na mashambulizi mawili tofautio ambapo wanjeshi waliuawa katika eneo la milimani la Galgalo.
Kwa mujibu wa taarifa za kundi la Al shabaab waliwauawa zaidi ya wanajeshi 30 wa serikali kabla kutoweka katika milima hiyo.
Wapiganaji wengi wa Al Shabaab wameripotiwa kukimbilia eneo la Puntland katika miezi ya hivi karibuni huku jeshi la Somalia pamoja na wanajeshi wa Muungano wa Afrika kudhibiti Kusini mwa Somalia.
 chanzo:BBC

0 comments:

Post a Comment