.

.
Saturday, December 1, 2012

10:26 AM

Nahodha wa Rwanda, Haruna Niyonzima akimtoka mchezaji wa Eritrea, katika mchezo wa mwisho wa Kundi C, Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge uliofanyika Uwanja wa Lugogo jioni hii. Rwanda ilishinda 2-0 na sasa itavaana na Tanzania katika Robo Fainali.

Na Mahmoud Zubeiry, Kampala
TANZANIA Bara, Kilimanjaro Stars itacheza na Rwanda katika Robo Fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge Jumatatu kwenye Uwanja wa Lugogo kuanzia saa 8:00 mchana, wakati Zanzibar itacheza na Burundi saa 10:00 jioni.
Robo Fainali nyingine zitachezwa Jumanne Uwanja wa Mandela, Namboole, kati ya Kenya na Malawi saa 10:00 jioni wakati wenyeji Uganda watacheza na Ethiopia saa 1:00 usiku.
Katika mechi za leo, Bara iliilaza Burundi mabao 7-0 katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Lugogo mjini hapa.
Matokeo hayo yanaifanya Bara itimize pointi sita baada ya kucheza mechi tatu na sasa, wakishinda mbili na kufungwa moja.
Burundi imemalizaa kileleni mwa Kundi B, kufuatia ushindi wa 1-0 dhidi ya Sudan, bao pekee la Chris Nduwarugira.
Rwanda imeifunga Eritrea 2-0, mabao ya Tadi Etikiama na Tumaine Ntamuhanga, huku Malawi ikiilaza Zanzibar 2-0.  
Stars, inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager leo ilionyesha kandanda safi na kusisimua mashabiki wa Tanzania waliokuja kuoiunga mkono hapa, akiwemo Mbunge wa Kondoa Kaskazini, Alhaj Juma Nkamia.
Iliwachukua sekunde 48 tu Stars kupata bao la kwanza, kupitia kwa mshambuliaji wa Simba SC, inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premum Lager pia, Mrisho Khlfan Ngassa aliyewazidi ujanja mabeki wa Somalia.
Kabla hawajakaa vizuri, Somalia walipachikwa bao la pili, dakika ya 23 lililofungwa na Ngassa tena, aliyeunganisha kona nzuri ya Issa na Rashid.
John Bocco ‘Adebayor’ alifunga bao la tatu katika mchezo wa leo na la tatu kwake katika mashindano haya dakika ya 26 akiunganisha kwa kichwa krosi ya Issa Rashid kutoka wingi ya kushoto.
Bocco tena aliwainua vitini mashabiki wa Tanzania kwa kufunga bao la nne kwa kichwa, akiunganisha krosi ya Ngassa dakika ya 41.
Ngassa alifunga bao la tatu katika mchezo wa leo dakika ya 44 na la tano kwa Stars baada ya kuuwahi mpira uliotemwa na kipa Hussein Abdallah kufuatia shuti kali la Salum Abubakar ‘Sure Boy Jr.’
Somalia ilipata pigo dakika ya 30, baada ya kipa wake namba moja, Mohamed Abdullah kuumia baada ya kugongana na Bocco na kutoka, nafasi yake ikichukuliwa na Hussein Abdallah. 
Kipindi cha pili Stars walirejea na moto wao na tena na kufanikiwa kupata mabao mawili zaidi yaliyotiwa kimiani na Ngassa yote dakika za 73 pasi ya Erasto Nyoni na 74 pasi ya Ramadhani Sinago ‘Messi’.
Kwa kufunga mabao matano, Ngassa sasa ameingia kwenye mbio za kaiti cha dhahabu akikwa anaongoza, akifuatiwa na Bocco ambaye ana manne hivi sasa.
Kocha wa Stars, Mdenmark Kim Pouslen baada ya mchezo huo, alisema aliwapongeza vijana wake kwamba wamejitahidi kucheza vizuri na akasifu pia hali nzuri ya Uwanja wa Lugogo kuwa ilichangia ushindi huo.
Mbunge Nkamia alisema kwamba amevutiwa na soka ya vijana leo na anaamini wana uwezo wa kurejea na Kombe nyumbani. Nkamia aliwapongeza wadhamini wa Stars kwa kuchangia mafanikio ya timu hiyo tangu waanze kuidhamini na akaomba Watanzania zaidi wajitokeze mjini hapa kuisapiti timu hiyo.
Waandishi wa Habari waliopo mjini hapa pia wamevutiwa mno na kiwango cha timu hiyo na kusema wana wana imani itafika mbali.
Wallace Karia, Mjume wa Kamati ya Utendaji ya TFF aliye hapa Uganda amesema amefurahishwa na kiwango cha timu na anaamini itafika mbali.
Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, wadhamini wa Kilimanjaro Stars, George Kavishe ametuma salamu za pongezi kwa ushindi wa leo na mafanikio ya kutinga Robo Fainali na kusema anatakia mafanikio zaidi timu hiyo.
Katika mchezo wa leo, kikosi cha Stars kilikuwa; Juma Kaseja, Erasto Nyoni, Issa Rashid, Shomari Kapombe, Kevin Yondan/Ramadhani Singano, Shaaban Nditi, Mrisho Ngassa, Salum Abubakar, John Bocco/Christopher Edrwad, Frank Domayo/Athumani Iddi na Amri Kiemba.
Somalia; Mohalim Abdullahi/Hussein Abdallah dk30, Ali Mohamed, Said Mahamud, Ali Dadir, Sadaq Abdikadir, Mohamed Salah, Abdikarim Abubakar, Abdallah Mohamed/Hamza Mukhtar, Ahmed Abdikadir Dahir/Muhad Hajji na Ali Ahmed Ali.  
MSIMAMO KUNDI A:
                      P   W  D   L    GF GA GD Pts
Uganda          3    3    0    0    6    0    6    9
Kenya            3    2    0    1    4    2    2    6
Ethiopia         3    1    0    2    2    3    -1  3
Sudan Kusini 3    0    0    3    0    7    -7  0
MSIMAMO KUNDI B:
                     P   W  D   L    GF GA GD Pts
Burundi         3    3    0    0    7    1    6    9
Tanzania       3    2    0    1    9    1    9    6
Sudan           3    1    0    2    1    3    -2  3
Somalia         3    0    0    3    1    13 -12 0
MSIMAMO KUNDI C:
                    P   W  D   L    GF GA GD Pts
Rwanda        3    2    0    1    5    2    3    6
Zanzibar       3    1    1    1    2    2    0    4
Malawi          3    2    0    1    5    4    1    6
Eritrea          3    0    1    2    2    5    -3  1
ROBO FAINALI
Desemba 3, 2012
Tanzania Vs  Rwanda   Saa 8:00 mchana    Lugogo
Zanzibar Vs   Burundi   Saa 10:00 jioni         Lugogo
Desemba 4, 2012
Kenya Vs Malawi           Saa 10:00 jioni         Namboole
Uganda Vs Ethiopia      Saa 1:00 usiku         Namboole

0 comments:

Post a Comment