.

.
Monday, December 3, 2012

2:37 PM
Aliyekuwa m'bunge wa jimbo la Arusha mjini Godbless Lema akihutubia katika moja ya mikutano yake jijini Arusha
USIKILIZWAJI wa uamuzi wa pingamizi za awali wa kesi ya rufaa iliyofunguliwa na aliyekuwa mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, (CHADEMA), leo inatarajia kujulikana hatma yake.
 Rufaa hiyo inayotarajiwa kusikilizwa mapema leo hii jijini Dar, na majaji watatu wakiwemo, Natalie Kimaro na Salum Massati itatoa maamuzi (hatma) juu ya ubunge wa aliyekuwa mbunge wa jimbo la Arusha mjini Godbless Lema.
Lema akiwajulisha wafuasi wa CHADEMA (hawapo pichani) juu ya uamuzi wa mahakama kuhamishia rufaa hiyo jijini Dar mara baada ya kutoka kusikiliza rufaa hiyo octoba 2 mwaka huu
awali mahakama ya Rufaa Tanzania, imekataa kuifuta rufaa iliyofunguliwa na aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini, Godbles Lema (CHADEMA) kwa maelezo kuwa upungufu uliyopo kwenye nakala ya hukumu ya Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, iliyotengua ubunge wake, hauwezi kuwa sababu.
Lema alikata rufaa mahakamani hapo, akipinga hukumu iliyotolewa Aprili 5 mwaka huu, na Jaji Gabriel Rwakibarila wa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha.
     

0 comments:

Post a Comment