.

.
Saturday, December 29, 2012

12:39 PM

Familia zilizoathiriwa
Familia zilizoathiriwa kwa mujibu wa Gazeti la Standard Nchini Kenya wakipekuwa mali yao baada ya maporomoko hayo ya Ardhi
Watu wanane wamekufa baada ya nyumba kadha kufukiwa na maporomoko ya ardhi katika eneo la bonde la Kerio, magharibi mwa Kenya, jana usiku.
Maporomoko ya ardhi yamesababishwa na mvua kubwa zilizonyesha katika bonde hilo. Eneo la Kerio pia limekumbwa na mafuriko kutokana na mvua kubwa inayonyesha.
Chama cha Msalaba Mwekundu cha Kenya kinasaidia jitihada za uokoaji na kutoa taarifa kwamba miili miili ya watu wanane imeonekana na watu wengine watano waliokolewa mapema leo.
Watu wengi hawana makaazi kutokana na nyumba zao kusombwa na maji au kufukiwa na maporomoko ya ardhi.
............xxx.............xxx.............xxx............

Wahamiaja haramu 18 wafariki Misri

Wahamiaji haramu
Wahamiaji haramu wakijaribu kuvuka baharini
Balozi wa Somalia nchini Libya Bwana Abdikani Mohamed Waeys amesema ana taarifa ya vifo vya raia 18 vilivyotokea kutokana na ajali ya lori nchini Libya.
Wasomali hao wanaotajwa kuwa wahamiaji haramu, 23 wameripotiwa kujeruhiwa huku wengine wakiwa katika hali mbaya.
Balozi Abdikani amesema lori hilo lililokuwa limebeba mifuko ya saruji walimokuwa wamejificha Wasomali hao, lilipinduka na kusababisha vifo, na kusema idadi yao walikuwa 120 wakiwemo wanaume na wanawake wote wakiwa ni Wasomali.
Katika miaka ya hivi karibuni idadi ya wahamiaji haramu ambao wamefariki wakijaribu kuvuka baharini imeongezeka.
chanzo ;BBC

0 comments:

Post a Comment