.

.
Tuesday, December 18, 2012

11:24 AM
 
Rais  Jacob Zuma wa  Afrika  kusini  amechaguliwa tena kukiongoza chama  tawala  cha  African National Congress (ANC).
Bw.  Zuma  ameshinda  kwa  karibu  kura 3,000, wakati  Makamu wake aliyekuwa pia akiwania nafasi hiyo Kgalema Montlante amepata  kura  chini  ya  1,000  katika uchaguzi  wa  uongozi  wa  chama  hicho  uliofanyika  leo.
Upigaji  kura  ulianza  asubuhi  ya  leo  katika  mkutano  wa ANC  wa  Mangaung, uliofanyika  katika  mji  ambao  pia unafahamika  kama  Bloemfontein.
Takriban wajumbe  4,000  wamepiga  kura  katika kinyang’anyiro  hicho  cha  uongozi  wa  juu  wa  chama cha  ANC.

0 comments:

Post a Comment