.

.
Sunday, December 23, 2012

11:15 PM
            mwenyekiti wa taifa chama cha demokrasia na maendeleo chadema Freeman Mbowe    akisalimiana na  laira Odiga huko nchini kenya. 
 
MAHASIMU wawili wa kisiasa nchini Kenya, Raila Odinga na Uhuru Kenyatta, wameingia katika mpambano wa kugombea urais nchini humo baada ya kila mmoja kupitishwa na muungano wa vyama vyao.
Raila ni Waziri Mkuu katika Serikali inayomaliza muda wake chini ya Rais Mwai Kibaki wakati Kenyatta ni Naibu Waziri Mkuu akimsaidia Raila.
Kenyatta alizindua kampeni zake mjini Mombasa, wakati Raila alikuwa mjini Nairobi na kila mmoja aliwaambia wafuasi wake kwamba anahitaji kupambana na ukabila na kujenga mshikamano wa wananchi wote wa Kenya.
Wajumbe wa vyama vya The National Alliance (TNA) na United Republican Party (URP) waliounda Muungano wa Jubilee walimpitisha Kenyatta kugombea nafasi hiyo na kumwacha, Musalia Mudavadi.
Awali ilikuwa iikifahamika wazi kwamba Kenyatta hakuwa na mpango wa kugombea nafasi hiyo na badala yake aliahidi kumwachia nafasi hiyo Mudavadi.
Mudavadi hakufanikiwa kupewa hata fursa ya kuwa mgombea mwenza wa Kenyatta na badala yake nafasi hiyo amepewa William Ruto.

Hatua hiyo imekuja siku mbili tangu Muungano wa Jubilee utangaze kuwa umemwondoa  Mudavadi na chama chake cha UDF katika muungano huo kwa makubaliano.
Akizungumza na waandishi wa habari nchini Kenya, kiongozi wa URP, Kenyatta alisema Mudavadi ataendelea na azma yake ya kusaka urais bila kuhusiana na Muungano wa Jubilee.
Kwa upande wa Muungano wa Cord, wao walimpitisha Raila kugombea akiwa na mgombea mwenza, Steven Kalonzo Musyoka ambaye ni Makamu wa Rais wa nchi hiyo hivi sasa.

Wakati Kenyatta akitangaza nia yake hiyo mjini Mombasa, Raila alijinadi jijini Nairobi na kusema kuwa wamejipanga kwa ajili ya kuondoa matatizo yanayoikabili nchi hiyo.
Raila alieleza kuwa atawaondolea Wakenya matatizo ya ajira na lindi la umaskini, hivyo aliwasihi kuunga mkono Muungano wa Cord ili waweze kujikwamua kiuchumi.

Katika mkutano huo  Kalonzo alisema wazi kuwa Wakenya wanatakiwa kuchukua fursa hiyo kumchagua Raila  kwa kuwa katika viwanja hivyo waliamua kumchagua Kibaki kuwa Rais, “Raila alisema Kibaki atosha sasa mimi nasema Raila anatosha”.
Kwa upande wake, Kenyatta alisema Wakenya wameteseka kwa muda mrefu na sasa ameamua kujituma ili kuwakwamua  katika lindi la umaskini  na shida.

Naye Ruto alisema hakuna Mkenya ambaye atakufa kwa njaa kwa sababu wataliendesha taifa hilo kwa roho safi bila ubaguzi wa ukabila.

0 comments:

Post a Comment