.

.
Monday, November 12, 2012

5:06 AM
Waandamanaji katika mji mkuu wa Athens

Bunge la Ugiriki limepitisha bujeti ya 2013 lenye orodha ya mapunguzo ya matumizi ambayo ni muhimu kwa nchi hiyo ili kuwashawishi wadhamini wa kimataifa kutoa fedha nyingine kama mkopo ili kuinusuru Ugiriki isifirisike.
Bajeti hiyo iliyopitishwa kwa kura 167 kwa 128, inanuia kupunguza matumizi ya serikali, mishahara na marupurupu.
Mbunge wa upinzani Evangelos Venizelos aliwaonya washiriki wenza wa Uropa kwamba wakichelewa kutoa mikopo kwa nchi hiyo, basi siyo Ugiriki tu itakayoaathirika bali eneo zima la Eurozone. "Nchi hii imefika ukingoni," alisema.
Wakati huohuo, kwenye mji mkuu wa Athens, zaidi ya watu 10,000 waliandamana nje ya bunge.
Inategemewa kuwa mwaka ujao kiwango cha uchumi wa taifa kitapungua kwa kiasi cha asilimia 4.5, huku deni la umma likitarajiwa kuongezeka.
chanzo:bbc

wakati bunge la ugiriki likijitahidi kuokoa uchumi wa nchi kwa hali na mali mbona Tanzania tuna.................kwa kuficha mabilioni nje? si bora tungeficha hata hapa nchini maana wengine tungeneemeka kwa mikopo na ingesaidia pia?

0 comments:

Post a Comment