.

.
Tuesday, November 20, 2012

10:24 PM
Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa habari Mkoa wa Arusha, Claud Gwandu pamoja na Mkurugenzi wa fedha na utawala wa umoja wa
vilabu ya waandishi wa habari nchini (UTPC), Jackson Uisso (kulia),  wakikagua moja ya vifaa vilivyotolewa msaada na umoja huo kwa APC juzi jijini Arusha.

Katibu Mkuu wa klabu ya waandishi wa habari Mkoa wa Arusha Eliya Mbonea (kushoto), akisaini nyaraka za makabidhiano ya
vifaa mbalimbali vya ofisi kutoka kwa umoja wa klabu za waandishi wa habari nchini UTPC jana katika ofisi za chama hicho jijini Arusha.
Anaeshuhudia kulia ni Mkurugenzi wa fedha na utawala wa UTPC, Jackson Uisso.

MUUNGANO wa Vyama vya Waandishi wa Habari nchini (UTPC) uimeikabidhi Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Arusha (APC) vifaa vyenye thamani ya Sh. Milioni 35.
Vifaa hivyo vilikabidhiwa jana Ofisa Utawala na Fedha wa UTPC Jackosn Uiso katika ofisi za Klabu ya APC jijini hapa na kushuhudiwa na viongozi na baadhi ya wanachama.
Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo Uiso aliwahimiza viongozi kuhakikisha vinatumika kwa wanachama ikiwa ni pamoja na kuingizia fedha Klabu.
“UTPC inawahimiza mtumie vifaa hivi kwa uangalifu, lakini hakikisheni mnaweka utaratibu wa jinsi gani vitawaingizia fedha za Klabu badala ya kuendelea kuvifungia,” alisema Uiso.
Baadhi ya vifaa vilivyokabidhiwa ni pamoja na Mashine ya kudurufu, Televisheni ya Inchi 32, Kamera kubwa ya kisasa kwa ajili ya picha za mnato, mashine ya Projector, Desk Kompyuta na Laptop.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa APC Claud Gwandu aliwashukuru UTPC kwa kukabidhi vifaa hivyo na kuahidi kwamba vitatumika kwa uangalifu mkubwa.
“Vifaa hivi ni vya thamani na tunaahidi kuvitumia kwa uangalifu utakaoleta manufaa kwa Klabu na wanachama wake,” alisema Gwandu.
Naye Katibu Mkuu wa APC Eliya Mbonea kwa upande wake aliwashukuru UTPC kwa kufanyia kazi mawazo ya viongozi wa Klabu nchini waliopendekeza kutumiwa vifaa vinavyolingana na taaluma.
“Mapendekezo ya viongozi wa Klabu yamefanyiwa kazi, awali tulikuwa tunaletewa kamera ndigo zinazowapa wakati mgumu waandishi kupiga picha hususani viongozi wa kitaifa wanapokuja au tukio linapokuwa mbali,” alisema Mbonea na kuongeza:
“Mfano hii Kamera ya picha za mnato kweli hapa sasa hatuwezi kulalamika tena kwamba hatuna kamera ya kisasa kwani Kamera hii unaweza kupiga picha ukiwa mahali popote,” alisema. 
chanzo:libeneke la kaskazini blog

0 comments:

Post a Comment