.

.
Sunday, November 11, 2012

3:35 AM
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho akitia saini kitabu cha maombolezo ya kifo cha Mhashamu Baba Askofu Aloysius Balina wa Jimbo Katoliki la Shinyanga baada ya kuwasili kwenye Kanisa la Mama wa Huruma katika Parokia ya Ngokolo mjini Shinyanga kushiriki mazishi ya Askofu huyo, Jumamosi, Novemba 10, 2012.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa Mhashamu Baba Askofu Aloysious Balina wa Jimbo Katoliki la Shinyanga wakati wa mazishi wa Askofu huyo kwenye Kanisa la Mama wa Huruma, Ngokolo, mjini Shinyanga leo.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akiweka udongo kwenye kaburi la Askofu Aloysius Balina wakati wa mazishi ya Askofu huyo kwenye Kanisa la Mama wa Huruma, mjini Shinyanga.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akiweka shada la maua kwenye kaburi la Askofu Aloysius Balina wa Jimbo Katoliki la Shinyanga wakati wa mazishi ya Askofu huyo kwenye Kanisa la Mama wa Huruma, Ngokolo, Shinyanga

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameungana na mamia kwa mamia ya waumini wa Kanisa Katoliki kumzika Askofu wa Jimbo Katoliki la Shinyanga, Mhashamu Baba Askofu Aloysius Balina yaliyofanyika kwenye Kanisa la Mama wa Huruma, Parokia ya Ngokolo, mjini Shinyanga. 
 Rais Kikwete ambaye amekwenda Shinyanga akitokea Dodoma ambako anaendesha vikao muhimu vya Chama cha Mapinduzi amewasili kwenye Kanisa hilo kiasi cha saa sita mchana kwa ajili ya mazishi ya Askofu Balina ambaye alifariki dunia Novemba 6 mwaka huu katika Hospitali ya Rufaa, Mwanza kwa ugonjwa wa saratani. 
 Mara baada ya kuwasili Kanisani hapo, Rais Kikwete ametia saini kitabu cha maombolezo na kujiunga na viongozi wa Kanisa hilo na wa Serikali akiwamo Rais Mstaafu Mheshimiwa Benjamin Mkapa na Mama Maria Nyerere kushiriki katika mazishi ya kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki.

0 comments:

Post a Comment