.

.
Tuesday, November 13, 2012

9:58 PM
bwana Bill Mushi akihutubia kwenye mahafali hayo
                                Waandishi wa habari wametakiwa kuandika suluhisho ya matatizo mbali mbali yanayoikumba jamii ya watanzania na siyo kila siku kukazania kuandika tu mapungufu yanayosemwa juu ya viongozi wa serikali.
Rai hiyo imetolewa na bwana Bill Mushi alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kwenye mahafali ya tano ya chuo cha uandishi wa habari na utangazaji (AJTC) kilichopo mbauda mkoani Arusha.
Bwana Bill alisema kuwa mara nyingi waandishi wa habari hupenda zaidi kuandika mapungufu mbali mbali yanayojitokeza kwa viongozi wetu na kuwa changamoto kwa jamii bila kujali sababu hali ambayo imekuwa kikwazo kwa baadhi wa watendaji na kushindwa kufanya kazi kwa ufanisi zaidi.
“ Kweli kuna changamoto nyingi zinazoikumba jamii hasa ajira kwa vijana, lakini si vema kukazania kuandika kuwa kuna tatizo la ajira, ni lazima mda mwingine make na kufikiri nini cha kuandika ambacho kitakuwa ni suluhu la tatizo hilo”Alisema Bill.
Pia aliwataka kutoandika zaidi habari za kuripoti badala yake wajikite zaidi katika habari za kiuchunguzi ili kuisaida nchi yetu kujua mambo mengi mtakayoyaibua ikiwemo kuibua vyanzo mbalimbali za mapato katika jamii.

Mkurugenzi wa chuo cha AJTC Joseph Mayagila (aliyesimama) ikimkaribisha mgeni rasmi Bill Mushi (aliye upande wake wa kulia) na anayefuata ni Afisa tawala wa chuo hicho Bwana Elifuraha Samboto akisikiliza kwa amkini ukaribisho huo
                                                      
Naye mkurugenzi wa chuo hicho cha Arusha Journalism Trainning College (AJTC) Bwaba Joseph Mayagila alisema kuwa wahitimu hao 75 wamemaliza kozi tofauti tofauti ikiwemo cheti cha juu cha uandishi wa habari, stashahada, na stashahada ya juu ya uandishi wa habari pamoja na uhusiano wa kimataifa.

Pia Mayagila aliongeza kuwa tofauti na kozi hiyo iliyowafanya wanafunzi hao kuja chuoni hapo pia wanatoa elimu ya ujasiriamali itakayoweza kuwasaidia wahitimu kukabiliana na tatizo la ajira wakiwa mitaani ikiwemo kutokuangalia zaidi kuajiriwa badakla yake wabuni vyanzo vyao wenyewe vya mapato na wajiajiri kiujasiriamali.
Chuo hicho pekee chenye kutoa mafunzo ya hali ya juu ya uandishi wa habari na utangazaji inayoendana na soko la jumuiya ya Afrika mashariki pia inatoa mafunzo ya kompyuta, ujasiriamali na kukuza fani mbali.

Baadhi ya wahitimu wakiwa na nyuso za tabasamu baada ya kuhitimu mafunzo
Katika burudani:         AJTC mamong'o pia wapo
                              

0 comments:

Post a Comment