Rais Obama akiwa na familia yake kabla ya kuwahutubia wamarekani baada ya ushindi.
Rais Obama amemshinda mpinzani wake Mitt Romney kwa wingi wa kura za
majimbo ambapo amepata jumla ya kura 303 dhidi ya kura 206 alizopata
Romney,ambaye hata hivyo ameshinda Obama kwa kura za wananchi kwa
asilimia 50 ya kura huku Obama akiambulia asilimia 49.
Rais
wa Maerkani Barack Obama amewashukuru wamarekani kwa kuonesha imani juu
ya uongozi wake na kumpa ridhaa ya kuongoza tena taifa hilo kwa muhula
wa miaka minne ijayo.
Katika
hotuba yake baada ya kutangazwa kushinda rais Obama amesema kuwa kwa
sasa anarejea ikulu akiwa na malengo thabiti na mwenye ari zaidi ya
awali kwa lengo la kuwatumikia raia wa taifa hilo.
Obama amesema kuwa haijalishi tofauti zozote zilizopo kwa wamarekani
bado kwa pamoja inawezekana kulifikisha taifa hilo mbele zaidi katika
suala la maendeleo na usalama, ili kuhakikisha ndoto za wamarekani wote
zinatimia.
Aidha rais Obama amemshukuru mpinzani wake Mitt Romney kwa kampeni
zenye ushindani na kwamba ataendeleza ushirikiano na gavana huyo ili
kuliwezesha taifa hilo kusonga mbele kwa manufaa ya wamarekani wote.
Rais Obama amemshinda mpinzani wake Mitt Romney kwa wingi wa kura za
majimbo ambapo amepata jumla ya kura 303 dhidi ya kura 206 alizopata
Romney,ambaye hata hivyo ameshinda Obama kwa kura za wananchi kwa
asilimia 50 ya kura huku Obama akiambulia asilimia 49.
0 comments:
Post a Comment