.

.
Monday, November 12, 2012

4:52 AM
Wanavijiji nchini Kenya kaskazini wanahofia kuzuka kwa mapigano zaidi baada ya takriban polisi 29 kuuwawa mwishoni mwa wiki.
Polisi hao walivamiwa walipokuwa wanajaribu kurudisha ng'ombe waliokuwa wameibwa.

"Hali ni ya wasiwasi sana, huku walinda usalama waliojihami kwa silaha wakipiga doria vijijini," kiongozi mmoja wa kidini huko Kaunti ya Samburu alisema.
"Tunahofia kwamba maafisa wa ulinzi waliojawa na hasira huenda wakawashambulia wananchi wasio na hatia kwani waliowaua polisi hao wameshatoroka," alidokeza kiongozi huyo.
Aidha alisema kwamba kungali kuna miili mingine ambayo haijapatikana.
Wasamburu na Waturkana huibiana mifugo mara kwa mara. Pia hupigania maeneo ya lishe kwa mifugo na maji.
Kulingana na waandishi habari wa Kenya, majuma mawili yaliyopita watu 12 waliuwawa katika tukio kama hilo karibu na mahala hapo.
chanzo: BBC

0 comments:

Post a Comment